Waombolezaji wakiwasili msibani.
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Amina Ngaluma, amezikwa leo mchana katika Makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam, kuashiria kuwa sura au sauti ya mkali huyo haitosikika wala kuonekana tena.
Ngaluma aliyefariki nchini Thailand, mwili wake uliletwa jana usiku, ambapo wadau na mashabiki wa muziki wa dansi Tanzania, walipata fursa ya kushiriki katika mazishi yake.
Tofauti na wakati wa mapokezi ambapo wanaamuziki walishindwa kuhudhuria, jana katika mazishi hali ilikuwa nzuri kwa wadau wengi kujitokeza.
Waombolezaji (akinamama), wakiwa katika msiba huo.
Waombolezaji wakisubiri taratibu za mazishi.
Kutoka kushoto, Mzee Kitime, Rashid Sumuni na Ali Choki, wakipata chakula msibani hapo.
Jenenza lenye mwili wa marehemu Amina Ngaluma, likiingizwa kwenye Makaburi tayari kwa ajili ya mazishi leo. |
No comments:
Post a Comment