TANGAZO


Tuesday, May 13, 2014

UN yalaaani shambulizi Somalia



Mji wa Baidoa ulikombolewa na serikali kutoka kwa Al Shabaab miaka 2 iliyopita
Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi baya sana la kujitoa mhanga lililotokea eneo la Kati mwa Somalia Jumatatu.
Taarifa kutoka kwa Muungano wa Afrika imesema kuwa watu 19 walifariki katika shambulizi hilo lililotokea mjini
Baidoa mnamo Jumatatu.
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, alisema kuwa alishtushwa sana na ukubwa wa mlipuko huo, na kuwataka wale waliotekeleza shambulizi hilo kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mji wa Baidoa ulikombolewa na serikali kwa usaidizi wa wanajeshi wa Muungano wa Afrika kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab miaka miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment