TANGAZO


Sunday, May 11, 2014

Mkulima auteka msafara wa Kinana wilayani Nzega

*Auelekeza shambani kwake


Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii cha chama hicho baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega, Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiwapungia mikono wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega
 Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakiti wa mwendelezo wa ziara ya  katika Mkoa wa Tabora.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Mohamed Kashindye mmiliki wa shamba la kumwagilia la mpunga  alipozuiwa kuondoka na msafara wake kulazimishwa kwenda  shamba lake alipokuwa akitaka kuondoka baada ya kukagua mradi wa maji wa Bukene, wilayani Nzega. Mkulima huyo alimuomba Kinana kufanya hivyo licha ya shamba lake kutokuwemo kwenye ratiba ya ziara ya kiongozi huyo. Kinana alikubali kukagua shamba hilo na kumpongeza Kashindye kwa kilimo hicho.
Kinana akishuka kwenye tanki  alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, wilayani Nzega leo.
Mahasimu wa kisiasa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Hussein Bashe (kushoto) akikumbatiana na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hamis Kigwangalah, walipokutana wakati Kinana akikagua mradi wa maji katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, Nzega.
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Nzega, Samweli Buyigi alipokuwa akikagua chujio la maji mjini Nzega leo
Akinamama, wanachama wa CCM wakichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya kufyatua matofali katika mradi wa akina mama uliofadhiliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega leo.
Kinana akibeba tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akina mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nanuye akisaidia kufyatua tofali.
Vijana wakitumbuiza kwa ngoma ya zeze walipokuwa wakimlaki Kinana katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Itobo.

Mbunge wa Jimbo la Bukene, akibebwa na wananchi ikiwa ni ishara ya kupendwa wakati wa ziara ya Kinana katika jimbo hilo.
Sehemu ya umati uliofurika kwenye mkutano wa CCM Kata ya Bukene.
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kukemea kitendo cha wana Ukawa kuwatukana vingozi waasisi wa muungano. (Picha zote na Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment