*CCBRT,
Vodacom Foundation na UNFPA kusaidia kampeni za kukuza uelewa wa jamii wa
kupambana na fistula
* Mabalozi 100 wa kijamii kuendesha warsha za wazi kueneza ujumbe “Fistula Inatibika”
Baadhi ya wakazi wa Tandika sokoni jijini Dar es Salaam, wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia”, wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika kwa ushirikiano wa wadau wa CCBRT, UNFPA na Vodacom Foundation. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani. Mmoja wa wasanii wa kundi la “Mpoto Theater”akigawa vipeperushi kwa Mariam Khamis vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia”, wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika kwa ushirikiano wa wadau wa CCBRT, UNFPA na Vodacom Foundation.Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani.
Kikundi cha wasanii wa muziki wa kiasili cha “Mpoto Theater”, wakitumbuiza na kuonesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani, zilizoandaliwa na CCBRT, UNFPA na Vodacom Foundation.
Wakazi wa Mbagala mwisho jijini Dar es Salaam Bi.Fatuma Ali(kushoto)na Khadija Rajabu wakiwa wakionesha vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
Msaani wa muziki wa kugani Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Mbagala rangi tatu kwa njia ya kugawa vipeperushi vyenye ujumbe wa “Fistula inatibia” wakati wa kampeni ya kutoa elimu kwa Umma juu ya tatizo hilo kuwa linatibika. Kampeni hizo zinafanyika nchi nzima katika kuaziamisha siku ya Fistula duniani na ratibiwa na CCBRT,UNFPA na Vodacom Foundation.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Leo Mei 23, 2014 Mabalozi 100 wa CCBRT, wataendesha
mafunzo ya wazi sehemu mbalimbali nchini yenye lengo la kuzijengea jamii uelewa
kuhusu fistula na kuwataka wanawake wenye matatizo hayo kujitokeza kupata
matibabu.
Wiki iliyopita, mabalozi 100 kutoka mikoa 25 Tanzania walihudhuria
mafunzo ya namna bora ya kuendesha simian hizo za kijamii kwa mafanikio pamoja
na kuwezeshwa vifaa vya kazi tayari leo kwa sauti moja iliyoungana watu hao 100
wanasambaza ujumbe wa “Fistula inatibika.”
Juhudi hizi ni matokeo
ya ushirikiano kati ya CCBRT na wadau wake ambao wote kwa pamoja wameweka azima
ya dhati ya kupambana na fistula na kumaliza tatizo hilo hapa nchini.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans alisema “ Maelfu ya
wanawake sehemu mbalimbali hapa nchini wanaishi maisha ya aibu na kutengwa
kutokana na kusumbuliwa na fistula bila kufahamu kwamba CCBRT na wabia wake
wanatoa matibabu bure ikiwa ni pamoja na kubeba gharama zote za usafiri wa
wagonjwa kufika Dar es salaam,malazi na chakula. Mabalozi wetu wa kijamii wapo
katika nafasi nzuri ya kuwafikia wanawake hao na kimisingi katika kipindi cha
mwaka mzima wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwafikisha kwetu wanawame hao kwa
matibabu. Leo tunawaomba wachukue hatua za ziada na tunaimani kuwa wakiwa na
nguvu mpya katika mikakati yetu ya kueneza ufahamu kwa jamii kuhusu fistula watawashawishi
wanawake wengi zaidi kutoka mafichoni.”
Mtandao wa mabalozi
wa CCBRT hutumika kuwabaini na hatimae kuwasafirisha wanawake wenye tatizo la
fistula kwa ajili ya matibabu. Pindi balozi wa fistula anapombainisha na
kumthibitisha mgonjwa hufanya mawasiliano na CCBRT kupitia nambari maalum
ambayo ni bure kwa wateja wote wa Vodacom na baada ya hapo CCBRT hufanya utaratibu
wa kutuma fefha za nauli zinazotumwa kwa njia ya M-pesa na hapo mwanamke mwenye
fistula huanza safri kuelekea CCBRT Dar es salaam au kwenye moja ya hospitali
zinazofanya nazo kazi ya Kigoma, Arusha na Moshi.
Kwa kila mgonjwa
mmoja anaefikishwa hopsitali balozi wa CCBRT hupata Sh 10,000/- kama motisha
kwa kusaidia kumaliza tatizo la fistula Tanzania.
Kwa sasa mtandao wa
mabalozi wa fistula unafikia mabalozi 500 wanaofanya akzi kwa utaratibu w
akujitolea wakifikisha hopsitali
wagonjwa wapatao 2,000
“Kutumika kwa
tekonolojia ya Vodacom kumesaidia kupunguza vikwazo kwa wanawake wanaotafuta
matibabu na ni moja kati ya ubunifu mkubwa kwenye sekta ya afya kuwahi kushuhudiwa
hapa Tanzania. Urahis wa kutumia huduma za kifedha za simu ya mkononi umeokoa
heshima ya maelfu ya wanawake walio masikini na waliotengwa hapa nchini kwa
sababu tu ya fistula. “Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw Rene Meza na
kuongeza
“Ubia wa Vodacom
Foundation na CCBRT umekuwa ukiimarika siku hadi siku na tunajivunia kufanya
kazi na wabia wetu mahiri katika kuadhimisha siku moja ya juhudi zetu pana za
kumalzia fistula hapa nchini.”
Siku ya kimataifa
ya kutokomeza fistula huadhimishwa Mei 23 ya kila mwaka kutambua umuhimu wa juhudi
za kumaliza tatizo hilo na pia kuonesha nia ya dhati ya Umoja wa Mataifa kwa
juhudi zote zinazofanywa za kutibu na kukinga fistula duniani.
“Kama sehemu ya
jamii, tunawajibu wa kumaliza janga hili la kiafya na kiutu, Tunavyoadhimisha
siku hii leo, wote lazima tukubaliane
kwamba kumaliza fistula hakuhsu tu upasuaji kwa mgonjwa. Ukweli wa mambo ni
kwamba tunaweza kumaliza tatizo hili nchini kwa kuwekeza kimkakati kwenye
maeneo matatu ambayo ni kinga, matibabu na kuwarejesha katika maisha ya awali
ya kijamii wale waliowahi kuugua na kupona.
Ujumbe maalum
Una
mtu mwenye fistula? Ungependa kuwa balozi wa CCBRT? Piga CCBRT (bure kwa wateja
wote wa Vodacom) ili kupata taarifa zaidi au kumfikisha hospitalikwa ajili ya
matibabu mwanamke anaegua fistula 0800752227.
No comments:
Post a Comment