TANGAZO


Sunday, May 11, 2014

Chama cha ANC chapata ushindi mkubwa



Rais wa Africa kusini Jacob Zuma asherehekea ushindi wa chama cha ANC katika uchaguzi mkuu uliokamilika.

Tume ya uchaguzi nchini Afrika kusini imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumatano.
Imesema kuwa chama tawala cha ANC kilijipatia ushindi mkubwa wa asilimia 62.
katika hotuba yake kwa taifa Rais jacob Zuma amesema kuwa matokeo hayo ni ishara njema kwamba raia nchini humo wana imani na chama cha ANC na kwamba chama hicho kitatumia umaarufu wake kuimarisha maisha ya watu masikini nchini humo.
Amesema kuwa ushindi huo umeipa serikali yake uwezo wa kuimarisha ukuwaji wa uchumi pamoja na ubunifu wa ajira.

No comments:

Post a Comment