Benki ya Barclays ya Uingereza imepanga kupunguza wafanyakazi 19,000 ifikapo mwaka 2016, kati yao elfu kumi wakiwa wafanyakazi wa benki hiyo nchini Uingereza.
Ikiwa ni sehemu ya mkakati mpya, upande wa uwekezaji wa benki hiyo utapoteza wafanyakazi 7,000 kufikia mwishoni mwa mwaka 2016.
Barclays pia itaanzisha kitengo cha benki hiyo ambacho kitashughulikia kuuza au kuendesha idara ambazo si kitovu cha benki zitakazogharimu pauni bilioni 115.Benki ya uwekezaji ya Barclays imekumbwa na kudorora kwa uchumi wake kutokana na madeni ya serikali na kampuni.
Kiasi hiki kitahusisha pauni bilioni 90 za uwekezaji wa mali za benki ya Barclays na shughuli zake zote za kibenki barani Ulaya, zinazofikia pauni bilioni 16.
Matawi ya benki hiyo katika nchi za Hispania, Ureno, Italia na Ufaransa yatahamishiwa katika kitengo cha idara ambazo si mhimili wa benki ya Barclays.
Mabadiliko hayo yataipa Barclays uwezo wa uendeshaji wa shughuli za rejareja nchini Uingereza, matumizi ya Kadi ya Barclays na kitengo cha Biashara ya Afrika.
"Huu ni uamuzi mzito wa kurahisisha uendeshaji wa Barclays," amesema afisa mkuu wa benki hiyo Antony Jenkins.
"tutakuwa benki ya kimataifa yenye dira, ikifanyakazi katika maeneo ambayo tuna uwezo na yenye faida kwetu kiushindani."
No comments:
Post a Comment