Ofisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha kuwa kanuni na taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium Muhemu
akifafanua kwa waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa hiyo
katika kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi
pamoja na watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispa
hiyo Bi. Joyce Nsumba. (Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira kwa
kuwa jukumu la kila mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia kanuni za usafi
wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke
Bw. Willium Muhemu wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam.
Bw. Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka mikakati
madhubuti ya kuhakikisha kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za usafi wa
mazingira zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha mlipuko wa
magonjwa.
“Moja ya mikakati iliyowekwa na manispaa ya Temeke
ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi
ili kuzuia uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu huo
atachukuliwa uchafuzi wa mazingira” Alisema Bw. Muhemu
Naye Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Ernest
Mamuya alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa katika hali ya
usafi wakati wote wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya kubeba taka , kuwa
na dampo la kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka zinazolewa kwa
wakati.
Akitoa wito kwa wananchi Bw. Mamuya alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuzingatia kanuni za usafi katika ngazi za familia ili
kuunga mkono mpango wa manispaa katika utunzani wa mazingira.
Maafisa afya wa kata wanaendesha zoezi la ukaguzi wa
nyumba kwa nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya za mitaa husika
ili kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.
No comments:
Post a Comment