Benki
ya NMB imezindua rasmi tawi lake jipya mjini Kigoma. Uzinduzi wa tawi
hilo lililoko katika jengo la Bima barabara ya Lumumba katika jengo la
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulifanyika mwishoni mwa wiki. Aidha,
tawi hilo lililo mkabala na Soko Kuu la Kigoma, limelenga kutoa huduma
kwa watu binafsi na wakazi wengi wa maeneo hayo hususan wafanya biashara
ndogo ndogo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kigoma .Hafla hii ya uzinduzi ilifanyika
katika viwanja vya tawi la NMB Kigoma.Wakishuhudia ni Meneja wa NMB
Kanda ya Magharibi Bw. Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa
tawi la NMB Kigoma, Bw. Rogers Malang’u.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akipata maelezo kuhusu huduma
za ‘NMB Fast Track’ kutoka na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Bw.
Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa tawi la NMB Kigoma, Bw.
Rogers Malang’u. Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Abraham Augustine alisema “Tumekuwa
tukifanya jitihada za kuhakikishia kwamba benki hii inatoa huduma bora
kwa wateja wetu wengi. Katika juhudi hizi, tumekuwa tukipanua mtandao wa
matawi kuhakikisha kwamba tupo katika maeneo jirani na wateja wetu.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe, Bw. Charles Gichilu (kulia) akipata huduma kutoka
benki ya NMB. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani
Maneno. Tawi hili la Kigoma litakua likitoa huduma zote kuanzia kuweka
na kutoa fedha, mikopo, malipo kwa taasisi kubwa zikiwemo za serikali na
nyinginezo.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
NMB Karibu Yako
No comments:
Post a Comment