*Wajumbe kutoka Zanzibar, wamwaga vijembe na matusi
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Salmin Awadhi (kushoto) na Nassor Jazira, wakizunguza jambo wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda (kulia) na Ester Buluya, wakiteta jambo ndani ya ukumbi wa Bunge, wakati wa kikao cha kuchangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silma akichangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mbarouk Salim Ali akichangia mjadala huo, wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Chiku Abwao, akichangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, katika kikao hicho, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Joseph Mbilinyi 'Sugu', akichangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, wakati wa mjadala huo.
Wanafunzi wa Shule ya Sokondari ya Dodoma, wakiwa kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma kufuatilia michango ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Bunge leo.
Wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Tabora, wakiwa kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma kufuatilia michango ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Bunge leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsi na Watoto, Dk. Pindi Chama, akichangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, wakati wa mjadala huo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwalimu Izekiel Oluoch, akichangia mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, wakati wa mjadala wa vifungu hivyo, bungeni mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na Rita Mlaki wakizungumza jambo ndani ya Bunge, wakati wa mjadala wa Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), akisalimiana na wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma mkoani Tabora, wakati walipofika kulitembelea Bunge hilo, mjini Dodoma leo.
MJADALA wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Sura ya Kwanza na ya Sita leo, umeendelea huku wajumbe wengi wakionesha misimamo ya Vyama vyao kuliko kujali maslahi ya wananchi kwenye katiba hiyo.
Baadhi ya wajumbe walionekana kutupiana vijembe badala ya kuchangia kwa hoja vifungu vya sura hizo vya Rasimu hasa wale wa kutoka Zanzibar, waliodhihirisha kwamba wako kwenye bunge hilo kwa kupambana tu na sio kwa ajili ya Katiba.
Pande zilizokuwa zikipambana zilionekana ni kati ya CCM Zanzibar pamoja na CUF kwa upande mmoja.
Hata wale wajumbe kutoka Bara nao, baadhi yao walionekana kuingia kwenye mtego huo wa malumbano ya matusi yasiyo natija kwa wananchi wanaosubira katiba yao kwa hamu kubwa.
Kwa kweli ilikuwa ni mnyukano wa aina yake ambao kamwe hata wakati mwingine unaweza ukajiuliza hii Katiba mpya ni ya nini kama mambo yenyewe ndio hivyo.
Baadhi ya wachangiaji kwenye sura hizo, walidiriki hata kuwakashifu kwa matusi ya nguoni huku baadhi ya wajumbe wakinekana kuyafurahia matusi hayo na kuyaunga mkono na baadhi yao wakiwa ni viongozi wa Serikali.
Hata wale wasomi waliutupa usomi wao na kufumba macho na kisha kujiingiza kwenye hoja ambazo haziisaidii nchi kupata katiba yake.
Ni mengi yaliyojitokeza katika kuchangia vifungu vya Sura hizo, lakini lililokuwa zaidi ni hili la matusi yaliyokuwa yakishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo, linalotumia pesa za walalahoi bila hata kujali utumwa ulioko mbele yao, waliotumwa na wananchi wavuja jasho.
Hali kama itaaendelea hivyo bila kukemewa huko mbele linaonekana giza ambalo mwisho wake itakuwa ni sufuri tu.
No comments:
Post a Comment