Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa
wateja toka Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya mpango wa bohari hiyo kupanua
maghala ya kuhifadhi Dawa na Vifaa tiba kama moja ya hatua za kuboresha huduma zinazotolewa
na Bohari hiyo . Kushoto ni Mkurugenzi wa
Manunuzi wa Bohari hiyo, Heri
Mchunga.
Mkurugenzi wa Manunuzi Bohari ya Dawa (MSD), Heri Mchunga akielezea kwa waandishi wa habari jinsi Serikali inavyodhibiti wizi wa Dawa kwa
kuweka nembo maalumu ambapo hadi sasa tayari dawa 20 zimewekewa nembo hiyo.
Kulia ni Mkurugenzi wa shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja Bohari ya Dawa, Edward Terry.
Na Frank Mvungi-Maelezo
SERIKALI yajipanga kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa uhakikika
katika hosipitali zote za umma hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja wa Bohari ya dawa (MSD) Bw.Edward
Terry wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza Terry amesema kwa hivi sasa
Bohari ya Dawa imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa dawa zinafika kwa wakati
katika maeneo yote zinakohitajika kwa kuweka mfumo mzuri unahakikisha kuwa dawa zikifika
zinatumika kwa wananchi waliokusudiwa .
Akieleza Zaidi Terry alisema kuwa
mnamo mwaka 2010 walifanya majaribio ya utaratibu wa kupeleka dawa moja kwa
moja kwenye vituo vya afya ambapo utaratibu huu umeonyesha mafanikio makubwa
hivyo ni imani ya Bohari ya Dawa kuwa utaratibu huo utasaidia sana kuondoa
tatizo la upatikanaji wa dawa hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wa Kudhibiti upotevu wa dawa katika
vituo vya Afya na Hosipitali Terry amesema dawa zinazotolewa na Serikali
zitakuwa na alama maalum ya kuzitofautisha na zile zinazouzwa katika maduka
binafsi ili kuondoa tatizo la wizi wa dawa zinazosambazwa na Bohari ya Dawa
hapa nchini.
Kuhusu Faida za kuweka alama maalum katika dawa za Serikali
Terry amesema utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu upatikanaji wa
dawa mara wanapahitaji huduma hiyo katika hosipitali au vituo vya afya kwa kuwa
tatizo la wizi litakoma.
Kwa wale watakaobainika kujihuisisha
na wizi wa dawa za Serikali ,Terry
amesema hatua kali zitachukuliwa bila
kuwaonea haya na kutoa wito kwa wananchi kuwafichua wale wote wanaojihusisha na
wizo huo ili mkondo wa sheria uchukue nafasi yake.
Bohari kuu ya Dawa imefungua kituo
cha Kusambaza Dawa cha Muleba ,Mkoani
Kagera kitakachosaidia kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Geita na Kagera
kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu.
No comments:
Post a Comment