Walinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamewasindikiza zaidi ya waisilamu,1,200, kutoka katika mji mkuu wa CAR Bangui kutokana na tisho kwa usalama wao.
Waisilamu hao ni baadhi ya waisilamu waliosalia mjini Bangui ambao walilengwa kushambuliwa na wakristo katika mzozo wa wenyewe kwa wenyewe.
Waasi hao wa Seleka walituhumiwa kwa kuwashambulia wakristo na kuchochea ghasia hizo zaidi. Gasia zilizozuka hata hivyo zilikuwa za kulipiza kisasi.Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu waasi wa Seleka, kupindua serikali mwezi Machi mwaka jana.
Pia kulikuwa na ripoti kwamba watu 22 wakiwemo machifu 15 na wafanyakazi wa shirika la Medecins Sans Frontieres (MSF), waliuawa mjini Nanga Boguila.
Mauaji hayo yalifanyika siku ya Jumamosi wengi wa waathiri wa wakiuawa wakati kliniki ya shirika hilo iliposhambuliwa.
Punde tu msafara huo ulipoondoka mjini Bangui, watu walivamia nyumba na majumba ya biashara yaliyokuwa yanamilikiwa na waisilamu hao na hata pia kuvamia msikiti.
"hatukuwataka waisilamu hapa na wala hatutaki msikiti wao,'' alisema mvamizi mmoja kwa jina Guy.
Waisilamu wachache sana wamebaki mjini Bangui lakini maelfu wametoroka katika siku za hivi karibuni, huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda.
Shirika la Amnesty International limetuhumu walinda amani kwa kukosa kuzuia mauaji ya halaiki.
No comments:
Post a Comment