Mfuko wa Mawasilisno kwa
Wote, umeanza rasmi zoezi la utekelezaji mradi wa "School Disability
Connectivity Project" wenye lengo la kuzisaidia shule za umma zenye watu
wenye mahitaji maalumu, kupata vifaa vya TEHAMA na huduma za mtandao wa
Internet kwa matumizi ya walimu na wanafunzi lli kujifunzia na kujiletea
maendeleo.
Utekelezaji huo,
umeanzia katika Shule ya Msingi ya Buguruni Wasiosikia, yenye watoto wenye
mahitaji muhimu ya kutosikia, ambapo Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, kwa
ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Avanti Communications, ya nchini
Uingereza, wamepewa computes 10 za kisasa zilizounganishwa na Mtandao wa Iterneti
unaitumia mitambo ya Satelaiti.
Akizindua
mpango huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiano, Sayansi na Technolojia, Dr.
John Mngodo amesema Serikali inatambua kwamba shule nyingi za watu wenye
mahitaji maalum, zinadahili wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali mchini Tanzania,
hivyo basi mradi huu utanufaisha jamii kubwa ya Watanzania kwa ujumla.
Dr. Mngodo,
ametoa rai kwa uongozi wa Shule hiyo ya Buguruni Wasiosikia, kuvitunza na
kuvihudumia vizuri vifaa hivyo ili
viweze kudumu kwa muda mrefu na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ili
kutimiza azma ya serikali kuwawezesha
watu wenye mahitaji maalum, kuweza kujiendeleza na kujiletea maendeleoi yao na ya
taifa kwa ujumla.
Ofisa
Mtandaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Umma, Peter Ulanga, amesema pamoja na
majukumu mengine ya Mfuko wa Mawasiliano Kwa Umma, mfuko huo pia unalo jukumu
kutambua watu wenye mahitaji muualum na kuwasaidia, hivyo wakaanzisha mradi huo
wa "School Disability Connectivity Project" unaohusisha shule 25 nchini Tanzania, ambapo kila
shule itapatiwa compyuta 10 za kisasa na meza zake, na kwa ushirikiano na
kampuni ya Avanti Communications, kila shule itaunganishwa na mtandao wa
internet kupitia satelait dish
Peter Ulanga
amesema Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, umeziainisha shule 25 za umma za watu
wenye mahitaji muhimu zitakazopatiwa vifaa vya TEHEMA, ila itekelezaji
utafanyika kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza, itazihusisha shule kumi. zikiongozwa
na Shule hiyo ya Buguruni Wasio sikia, shule nyingine ni Shule ya Uhuru
Mchanganyiko, Shule ya Msingi Msimbazi, Shule ya Msingi Mbuyuni, Shule ya
Msingi Kisiwandui, Shule ya Mazoezi ya Kufundishia Patandi, Mpilipili Maalum,
Shule ya Msingi Dumila, Shule ya Msingi Manyoni na Shule ya Mtanga Maalum
Kwa upande
wake, ofisa Mtendaji Mkuu wa Avanti Communications, David Williams, amesema,
kampuni yake inajisikia faraja sana, kuisaidia Tanzania kutoa fursa kwa watu
wenye mahitaji maalum, kuunganishwa na mtandao wa mawasiliano ya iterneti
kupitia kampuni yake na kusisitiza itaendelea kuwa tayari kushirikiana na
serikali ya Tanzania, katika miradi mingine mbalimbali ya mawasiliano kupitia
mfuko wa mawasiliano kwa umma!.
No comments:
Post a Comment