Frank Mvungi
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa na wakala huo.
Walwa alisema kuwa wakala huo umeweza kuongeza kiasi cha nafaka zilizonunuliwa kutoka kwa wakulima kutoka tani 61,587.784 mwaka 2008/2009 hadi tani 219,377.282 mwaka 2013/2014 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa mifumo ya utendaji wa wakala huo.
“Hadi kufikia Desemba 31 mwaka 2013 wakala ulinunua tani 219,377.282 za nafaka sawa na asilimia 110 ambapo tani 218,878.600 ni mahindi na tani 498.682 ni mtama” alisema Walwa.
Aliongeza kuwa wakala umeingia makubaliano ya mashirikiano ( Memorandum of Understanding(MOU) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuwahakikiishia wakulima soko la uhakika.
Katika kutekeleza makubaliano na WFP Walwa alisema kuwa wakala umeuza tani 80,000 mwaka 2011/2012 ambapo kwa sasa wakala unaendelea kutekeleza mkataba mwingine wa kuuza tani 23,000 kwa mwaka 2013/2014.
Katika hatua nyingineWalwa alisema kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi ya nafaka kutoka kwa wananchi, ajira za muda kwa wananchi takribani 3000 zizizalishwa na makundi mbalimbali ya wananchi wakati wa kukusanya nafaka tatika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula umepanga kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 241,000 za Sasa hadi tani laki 400,000 ifikapo mwaka 2016 na Tani 700,000 ifikapo mwaka 2024.
No comments:
Post a Comment