Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi
akimkabidhi hundi ya sh. milioni 2 Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Beatrice Mugula kwa ajili ya wagonjwa wa saratani watoto
waliolazwa katika hospitali hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB,
Noves Moses. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi (wa
pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa nguo, madaftari, sabuni, vitabu
vya watoto, Meneja wa jengo la watoto katika hospitali ya Muhimbili, Praxeda
Chenya kwa ajili ya kusoma vikiwa na thamani ya sh. milioni moja, ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB, Noves
Moses na wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Beatrice Mugula. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam,
mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa TPB wakiweka sawa zwadi kabla ya kuzikabidhi.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta na watoto waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika picha ya Pamoja.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakipanga bidhaa kwa ajili ya kuwakabidhi watoto waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam jana wakati walipofika kutoa msaada kwa watoto hao.
No comments:
Post a Comment