Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka
Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi ya maafisa wa idara mbali mbali za Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wakiwa katika kikao
cha utekelezaji Mpango kazi wa Robo tatu ya mwaka Julai-Machi
2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo
asubuhi,mwenyekiti wake akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amerejea wito wake wa kuzitaka Wizara na Idara za Serikali kutilia mkazo
kazi za utafiti ili kusaidia utekelezaji wa majukumu ya msingi ya
Wizara na Idara hizo.
Amesema
dhamira ya Serikali ya kuongeza fedha za shughuli za utafiti katika
bajeti ya Serikali imelenga katika kuhakikisha kuwa Wizara na Idara za
Serikali zinafanya tatifi ambazo matokeo yake yatakuwa chachu katika
utekelezaji wa majukumu yao ya msingi.
Dk.
Shein amesema hayo leo wakati alipokuwa akihitimisha mjadala wa Taarifa
ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa
kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2013/2014 katika mkutano
uliofanyika Ikulu.
Kwa
hiyo ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kukamilisha
utafiti wa ufikiaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu ambapo matokeo yake
yamekuwa msingi wa kuandaa Sera ya Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu.
Katika
kikao hicho ambacho kilihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais Balozi
Seif Ali Iddi, Mhe Rais alihimiza suala la vipaumbele vya Wizara na
Idara kwenda sambamba na majukumu ya msingi ya Wizara na Idara (core
functions) husika.
Kuhusu suala la msaada wa uendeshaji wa vituo vya vijana walioacha madawa ya kulevya nchini maarufu ‘Sober Houses’ Dk.
Shein amehimiza ushiriki wa wadau wengi zaidi huku akiitaka Ofisi ya
Makamu wa Kwanza wa Rais kuliangalia kwa upana zaidi suala hilo ikiwemo
kuandaa mpango maalum ambao utakuwa endelevu kuonesha msaada wa jamii
ikiwemo Serikali kwa vituo hivyo.
Katika maelezo yake ya awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi Fatma Abdulhabib Fereji alieleza kuwa katika kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 Ofisi yake imeweza kukamilisha utafiti wa kubaini huduma na fursa zinazopatikana kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na kukamilisha utayarishaji wa Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Aliongeza
kuwa shughuli nyingine ambazo Ofisi yake iliendelea kuzifanya kuwa ni
pamoja na kuendelea kusimamia marufuku ya mifuko ya plastiki pamoja na
kuendelea kusimamia uchukuaji holela wa maliasili zisizorejesheka.
Waziri
alieleza pia masuala yanayoendelea kutekelezwa na Ofisi yake ambayo
yanatarajiwa kukamilishwa katika mwaka ujao wa fedha kuwa ni pamoja na
Sera ya Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu, Sera ya UKIMWI, Kanuni ya
Sheria ya Dawa za Kulevya, Mkakati wa Kudhibiti Taka Ngumu na Mpango wa
Utekelezaji wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Hata
hivyo Waziri alieleza pia baadhi ya changamoto ambazo Wizara yake
inapambana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake zikiwemo za
uingizaji uliokithiri wa bidhaa chakavu, Ugumu wa jamii kufuata taratibu
za uvunaji maliasili zisizorejesheka, miundombinu isiyo rafiki kwa watu
wenye ulemavu na uelewa mdogo wa jamii juu ya watu hao.
Changamoto
nyingine ni ushiriki mdogo wa jamii katika mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya na unyanyapaa kwa wtu wenye virusi vya UKIMWI na watu walio
katika makundi maalum.
No comments:
Post a Comment