Bondia Mustafa Dotto (kushoto), akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati walipokuwa wakipima uzito leo jijini Dar es Salaam. Mabondia hao watazipiga katika ukumbi wa PTA, Sabasaba kesho, April 12 Jumamosi. Katikati ni Promota Jay Msangi. (Picha zote kwa hisani ya www.superdboxingcoach.blogspot.com) |
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto, utakaofanyika katika ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam kesho. |
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe', akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA, Sabasaba kesho, April 12, Jumamosi.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth, kutoka Thailand akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo, kwa ajili ya mpambano wao wa kesho, Jumamosi ya April 12, ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12, ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam na bondia Gavad Zohrehvand (kushoto) wa Iran. |
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi' Mawe na bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka Thailand wamepima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho Jumamosi ya April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mpambano huo, ambao utakuwa wa raundi kumi (10), utasindikizwa na mabondia Fransic Cheka ambaye atapambana na bondia Gavad Zohrehvand wa Iran, watakaozitwanga katika mpambano wa raundi 8.
Mbali na pambano hilo, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi, ambapo mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Mustafa Doto katika mpambano wa raundi sita pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayosindikiza mchezo huo ukumbini hapo.
Wakati wa mapambano hayo, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na sheria za mchezo huo, katika michezo ya mabondia maarufu, wakali wa mchezo huo, kama vile
No comments:
Post a Comment