TANGAZO


Friday, April 11, 2014

AJALI YA BASI LA SMART ILIYOTOKEA ENEO LA LUGOBA LEO

*Watu wawili wafariki dunia
*Wengi wajeruhiwa
*Wengine wapoteza fahamu
Basi la smart likiwa limepinduka eneo la Lugoba, Chalinze mkoani Pwani leo.
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo, akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata mshtuko.
Watu wawili wamefariki dunia kutokana na ajali ya Basi la Smart asubuhi ya leo.
Basi hilo lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Mombasa nchini Kenya, limeacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu wawili pamoja na kujeruhi abiria wanaokadiriwa kufika 20. 

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkata na Lugoba,  Barabara Kuu ya Chalinze-Segera, mkoani Pwani. (Picha zote, habari na DJ SEK BLOG)

No comments:

Post a Comment