* Mufti wa Zanzibar anena
* Ukawa wakutana
*Tanzania Kwanza waongea na waandishi
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki na Abdulsalaam Ameir, wakizungumza jambo, wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo kwa ajili ya kikao cha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Pili Katiba.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Abdallah Sadallah, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili Katiba, ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Askofu Mkuu mstaafu, Donald Mtetemela, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili Katiba, ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan wakijadili jambo wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakiteta jambo, huku wajumbe wenzao wakifuatilia michango mbalimbali vya sura hizo, ukumbini humo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, William Lukuvi, akizungumza wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusu shutuma zilizotolewa na wajumbe wenzake, upande wa upinzani za kueneza chuki na propaganda Kanisani, wakati wa akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita vya Rasimu ya Pili Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, wakiteta jambo, wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza katika mkutano wa umoja huo, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Ukawa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza kwenye kikao cha umoja huo,
kilichofanyika mjini Dodoma leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Mjumbe wa Ukawa na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu akizungumza katika mkutano wa Ukawa, uliofanyika mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Ukawa na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akizungumza kwenye mkutano huo wa Ukawa.
Mjumbe wa Ukawa na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Shibuda akizungumza katika mkutano wa Ukawa, uliofanyika mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Ukawa na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Moses Machari, akichangia mawazo yake kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Israel Natse, akizungumza wakati wa mkutano wa Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa), mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Kwanza na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Mkumba, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo, kuhusu wajumbe wenzao wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), waliotoka kwenye ukumbi wa Bunge na kususia bunge hilo. Kulia ni mjumbe wa umoja huo, Adam Malima.
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Kwanza na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Mkumba, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo, kuhusu wajumbe wenzao wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), waliotoka kwenye ukumbi wa Bunge na kususia bunge hilo. Kulia ni mjumbe wa umoja huo, Adam Malima.
Na Mwandishi wetu
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, wametakiwa kuzingatia kile kilichowapeleka Dodoma badala ya kuendeleza lugha za kejeli na matusi.
Mufti Mkuu wa Zanzibar , Sheikh Saleh Omar Kaabi, alielezea wasiwasi wake juu ya lugha za matusi zinazotumika katika mjadala huo ambao kwa kiasi kikubwa ni kinyume cha maadili ya dini zote ambazo zinahimiza kuheshimiana na kutodharauliana.
Mufti Kaabi alikemea tabia iliyojitokeza katika bunge hilo ambapo wabunge wamekuwa wakitukanana matusi ya nguoni na kusahau kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwao ni michango ambayo itaboresha rasimu hiyo ya katiba iliyo mbele yao .
Alisema kwamba Watanzania wanachotegemea kutoka kwa wajumbe hao ni hoja za msingi katika kutetea misimamo
Aliwataka wajumbe hao wavumiliane pale ambapo mjumbe atasikia hoja ambazo hazitamridhisha na ajiandae kujibu hoja hizo kwa dalili zenye mishiko.
Mufti Kaabi alikitakia kheri kikao hicho ili kifikie makubaliano juu ya katiba muwafaka inayotarajiwa na Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment