TANGAZO


Saturday, March 22, 2014

Waziri wa Afya, Dk. Seif Rashid atoa tamko 'Ugonjwa wa Kifua Kikuu'


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akitoa tamko kuhusu ugonjwa  wa kifua kikuu kwenye ukumbi wa wizara hiyo, mjini Dodoma jana. 
Meneja Mpango  wa Kudhibiti kifua kikuu na ukoma, Dk. Beatrice Mutayoba (wa kwanza kulia), Ofisa wa mpango huo, Dk.Deus Kamara (kushoto), wote  kutoka Dodoma, wakiwa katika mkutano huo. (Picha zote na Magreth Kinabo -Maelezo)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsilikiza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati alipokuwa akitoa tamko kuhusu ugonjwa  wa kifua kikuu   kwenye ukumbi wa wizara hiyo, mjini Dodoma jana.
Na Magreth Kinabo- Maelezo, Dodoma
IMEEZWA kuwa ugonjwa wa kifua kikuu  ni ugonjwa wa tatu ambao unasababisha vifo vya watu wengi hapa nchini  baada ya Malaria na Ukimwi.

 Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati akitoa tamko kuhusu ugonjwa huo, kwenye ukumbi wa wizara hiyo, mjini Dodoma, ambayo itaandhimishwa Machi 24, mwaka 2014 hapa nchini na nchi nyingine  duniani.

Aidha  kwa mujibu wa takwimu za Wizara hiyo zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa ugonjwa huo imeongezeka kutoka 11,000 mwaka 1980  hadi kufikia 63,892 mwaka 2012.
“ Utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya watu vya watu walioathirika na ukimwi vinatokana na kiifua kikuu.

“Tangu kuzuka kwa ukimwi hapa nchini, inakadriwa kuwa  asilimia10 ya waathirika wa ukimwi wana ugonjwa wa kifua kikuu na takribani asilimia 40 ya wagonjwa wa kifua kikuu wana maambukizo ya VVU. Hali hii inafanya kifua kikuu kuwa miongoni mwa changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ukimwi na katika vita vya kutokomeza umasikini hapa nchini,” alisema Dk. Rashid.

 Dk. Rashid   aliongeza kuwa  miongoni mwa sababu nyingine zinazochangia kuongezeka kwa idadi ni msongamano wa watu mijini, makazi duni  ya watu na wagonjwa kuchelewa kupata matibabu.

Aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwa “ Fikia  kila mtu, Gundua, Tibu na Ponya mgonjwa wa TB”.

Aliongeza kuwa sasa  takribani zaidi ya watu milioni mbili  hufariki kwa ugonjwa huo kila mwaka na asilimia kubwa ya vifo hivyo hutokwa Barani Afrika hususa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hivyo Tanzania ni nchi ya 14 kati ya nchi 22 zenye idadi kubwa  ya wagonjwa wa  ugonjwa huo duniani.

Alisema  miongoni mwa mikoa inayoongoza kuwa na  wagonjwa wapya   wengi  kwa takwimu za mwaka 2012  kati ya mikoa iliyoathirika kwa tatizo hilo  ni Dares Salaam 13,983,Mwanza 5,946 na Shinyanga 4,074.

No comments:

Post a Comment