*Awataka kuwa wazalendo, katika kuripoti habari za bunge hilo
Waandishi wa Habari, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, wakati alipokuwa akiifungua semina yao, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba. Mbele ni wajumbe wa bunge hilo, Hamis Dambaya na Yussuf Omar Chunda.
Waandishi wa Habari, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, wakati alipokuwa akiifungua semina yao, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba. Mbele ni waelimishaji wa semina hiyo, Kingunge Ngombale Mwiru, Dk. Ayoub Rioba na Mwalimu Bashiru Ally.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akizungumza, mjini Dodoma leo, wakati alipokuwa akiifungua semina ya waandishi kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akizungumza, mjini Dodoma leo, wakati alipokuwa akiifungua semina hiyo ya waandishi kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba.
Waandishi wa Habari, wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, wakati alipokuwa akiifungua semina yao, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Bunge), Deogratius Egidio, akizungumza mara baada ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, kuifungua semina hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akisalimiana na waelimishaji wa semina hiyo, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru na Dk. Ayoub Rioba, mara baada ya kuifungua semina hiyo, leo mjini Dodoma.
Mwelimishaji, Dk. Ayoub Rioba, akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, Mwalimu Bashiru Ally wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwasilisha mada kuhusu Rasimu ya Katiba mpya kwa mustakabali wa Taifa letu, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, Mwalimu Bashiru Ally wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwasilisha mada kuhusu Rasimu ya Katiba mpya kwa mustakabali wa Taifa letu, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, Mwalimu Bashiru Ally wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada hiyo, wakati wa semina hiyo ya waandishi wa habari, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akifafanua jambo, wakati akuwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina hiyo, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwasilisha mada hiyo, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina ya waandishi wa habari, kuhusu wajibu wao katika kuripoti habari za Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akifurahia jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada hiyo.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, wakati akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina yao hiyo.
Waandishi wa habari, wakimsikiliza mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, wakati akiwasilisha mada kuhusu mapendekezo ya Tume ya Katiba, kuhusu muundo wa Muungano, wakati wa semina yao hiyo.
Mwelimishaji, mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngombale Mwiru, akiwasilisha mada yake hiyo, mjini Dodoma leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa, akizungumza wakati wa semina hiyo, mjini Dodoma leo.
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
23/3/2014
WAANDISHI wa habari
nchini wametakiwa kuwa wazalendo , kuzingatia maadili na weledi wa taalum yao, wakati wote watakapokuwa wanaripoti habari za Bunge Maalum la Katiba ili
kuwasaidia wajumbe kutoa mchango utakaolinda tunu za taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana ,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati akifungua semina ya
waandishi wa habari juu ya wajibu wao katika kuandika habari za Bunge hilo
linaloendelea mjini Dodoma.
Alisema kuwa ni vema habari zinazoandikwa katika vyombo vya
habari mbalimbali hapa nchini wakaripoti habari ambazo zinasaidia kuimarisha na
kujenga misingi ya umoja , mshikamano , upendo na amani ,uwajibikaji na kulinda
muungano wa Tanzania.
“Tupo hapa tulipo ndani ya muungano wetu- Nchi moja na
Serikali mbili . Tusijitume wala tusitumike na kuwajibika kubomoa jamii yetu;
kwa kubeba masuala yasiyojengeka na kuyafanya ndio ya wananchi wanayahitaji
kuyajua na tukaacha yale ya kutuwezesha kuhimiza kuipata Katiba mpya na kusimamia
wananchi kusonga mbele na kujenga nchi yetu kwa pamoja na utulivu,”alisema Dkt.
Mukangara.
Naye Mwanasiasa Mkongwe ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum
la Katiba, Kingunge Ngombare Mwiru, amesema mchakato wa kupatikana kwa Katiba
lazima ufanikishe kupatikana kwa Katiba iliyo bora, kama haiwezekani, hakuna
haja ya kuendelea kupoteza fedha za wananchi.
Alisema kuwa ili
katiba iwe bora, lazima iboreshe muungano na umoja wa kitaifa baina ya Tanzania
Bara na Zanzibar.
Kingunge aliongeza
kuwa lengo la kuundwa kwa Katiba Mpya, ni kuondoa kero mbalimbali
zilizopo hivi sasa, ziwekwe kisheria zaidi na zisimamiwe na sheria mama ambayo
ni Katiba.
Mwanasiasa huyo mkongwe, alisema lengo la pili la kuundwa
kwa Katiba mpya, iwaletee wananchi mambo mapya ambayo yatawafaidisha wananchi.
Hata hivyo, alisema Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa
bungeni wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba, haijachambua kwa kina kero za wananchi zinazotakiwa kufanyiwa
kazi.
Alisema imeegemea zaidi katika mustakabali wa upatikanaji wa
vyeo na kuigawa nchi katika makundi ya serikali.
Kigunge alisema licha ya mafanikio ambayo nchi imeyapata
toka ipate uhuru, bado iko nyuma kimaendeleo, kwa kuwa ina serikali ambayo ni
tegemezi.
Alitolea mfano wa wajumbe wanaozungumzia mgawanyo sawa wa
madaraka uwekwe kwenye katiba na kuacha kero msingi zinazowakumba wanawake
ikiwemo ya ukeketaji.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Bashiru Ali alisema kuwa muundo wa Serikali tatu unaopendekezwa katika rasimu
ya Katiba Mpya unaiacha Serikali ya Shirikisho haina rasilimali ikwemo ardhi na
kuifanya ibaki inaelea hewani.
Alisema kwa mujibu wa mapendekezo yaliyomo katika rasimu
hiyo hakuna eneo linaloonyesha vyanzo vya mapato ya Serikali na Shirikisho
wakati linamiliki majeshi jambo ambalo linaloweza kusababisha machafuko.
No comments:
Post a Comment