TANGAZO


Sunday, March 23, 2014

Baada ya wananchi na wasomi kumlamu Rais Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Umoja wa Tanzania Kwanza wanena

* Wasema Rais Kikwete hajaingilia mchakato wa Katiba  

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Kwanza, Mjumbe waBunge Maalum la Katiba, Said Mkumba, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umoja wao huo, Ofisi za Bunge Mjini Dodoma leo. Kushoto ni Waride Bakari Jambu na katikati ni Charles Mwijage. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Kwanza, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Mkumba, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umoja wao huo, Ofisi za Bunge, Mjini Dodoma leo. Kulia kwake ni wajumbe wenzake wa Bunge hilo pamoja na baadhi ya waandishi wa habari. 
Mjumbe wa Umoja wa Tanzania Kwanza, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dk. Emmanuel Nchimbi, akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umoja wao huo, Ofisi za Bunge Mjini Dodoma leo. Katikati ni Mwenyekiti wa umoja huo, Said Mkumba na kushoto ni mjumbe wa umoja huo, Charles Mwijage. 

Na Magreth  Kinabo –Maelezo
UMOJA wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza, wasema kwamba hotuba ya Rais, Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi  wa Bunge Maalum la Katiba, haikuvuruga wala kuingilia mchakato wa kupata Katiba Mpya, bali alitoa maoni na ushauri kama kiongozi wa nchi.

Aidha, wajumbe hao, wamesema Rais hakuingilia kanuni za bunge hilo zilizopitishwa, hakubadilisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na hakupiga kura kwenye vifungu vya Katiba.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti  wa wajumbe hao, Said Nkumba katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa Bunge mjini Dodoma leo.

 Nkumba ambaye aliambatana na  baadhi ya  wajumbe wengine watano , ambapo alisema  hotuba  hiyo  imeweka wazi faida na hasara za mifumo yote ya Muungano  wa Tanzania kwa hoja ili Watanzania wawe na fursa pana ya kutafakari na kuamua.

“ Rais ametimiza kauli yake ya kushawishi kwa hoja na si kulazimisha,” alisema Nkumba.

Aliongeza kuwa alichokifanya Rais katika hotuba yake ni kama kiongozi mkuu wan chi mwenye hekima na busara na uchungu wa nchi yake na  kutambua dhamana aliyopewa na Watanzania wote bila kujali makundi ameelezea faida na hasara za mifumo ya Serikali  iliyowasilishwa kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba.

“Rais  katupa moyo na kutuhimiza tumalize kazi haraka na tuifanye kwa weledi huku tukiweka maslahi ya taifa mbele. 
Hata pale alipotoa maoni na ushauri kuhusu baadhi ya vifungu bado alisisitiza  kwamba umamuzi wa mwisho  ni wetu sisi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,” alisisitiza.

Nkumba alifafanua kuwa  dhana ya kuichambua na kuikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba  si kumdhalilisha Mwenyekiti wa Tume na Wajumbe wake. 

Hivyo msingi mzima wa kutolewa rasimu hiyo ni kwamba wananchi waichambue, kuikosoa ,kuboresha  na kuirekebisha na hata ikibidi kuibadilisha na mwisho kuipigia kura.

Alisema rasimu hiyo haikuletwa kama Msahafu wala Bibilia Na ndiyo maana zimewekwa hatua mbili  baada ya kazi ya tume kumalizika ,ambazo ni bunge hilo na kura ya maoni ya wananchi.

Aliwataka wajumbe wa bunge hilo kushirikiana ili kuweza kuifanya kazi hiyo.

Wajumbe wa bunge hilo wa Tanzania Kwanza wapo takribani 400 na watatoka katika makundi mbalimbali ambaomsimamo wao ni kushawishi kwa hoja na wala hawatalazimisha.

No comments:

Post a Comment