TANGAZO


Thursday, March 27, 2014

Watumiaji ardhi wawataka Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kuanza kuichambua Rasimu ya Katiba kama walivyotumwa na wananchi


Mwenyekiti wa Umoja wa Watumiaji Ardhi ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Maselle Nzingula Maziku (katikati) akitoa tamko la Umoja huo leo mjini Dodoma la kuwataka wanasiasa waliomo katika Bunge hilo kuacha mabishano na badala yake wafanye waliotumwa na wananchi ya kuichambua rasimu ya Katiba ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Wengine katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo ambye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Issa Suleman (kulia) na Kushoto ni Katibu wa Umoja huo na Mjumbe wa Bunge hilo Doreen Maro. (Picha na Maelezo-Dodoma) 



(Na Magreth Kinabo- MAELEZO,Dodoma)
UMOJA  wa Watumiaji wa Ardhi umewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuanza kuichambua Rasimu ya Katiba Mpya kama walivyotumwa na wananchi  ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuacha  kufanya kampeni za  kutafuta madaraka  kuliko kusimamia maslahi ya wananchi. 

Kauli hiyo imetolewa leo na  Mwenyekiti wa umoja huo , Dk. Maselle Maziku  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma .
Amesema  umoja huo utafanya kazi ya ya kuhakikisha unatetea haki za wakulima ,wafugaji na wavuvi katika mchakato wa kujadili Rasimu ya Katiba Mpya. 

 “ Tunawataka  wanasiasa watambue kwamba katikaBunge hili, hatukuja kufanya mabishano yasiyokuwa na mwisho na badala yake tunataka tuanze kuifanya ile kazi ambayo wananchi wametutuma ya kupitia  na kuichambua Rasimu ya Katiba,” alisema Dk. Maselle .

 Aliongeza kuwa umoja huo , umegundua kwamba makundi ya wanasiasa yanavuruga mchakato wa Bunge hilo  kwa kuendekeza misimamo yao ya kiitikadi na kusahau azma iliyowaleta  ya kuhakikisha Watanzania wanapata  Katiba Mpya isiyokuwa na upendeleo wa chama chochote  cha siasa.Hivyo  umeshoshwa na hali ya Bunge hilo kuonekana kuwa ni sehemu ya makundi ya wanasiasa.

No comments:

Post a Comment