TANGAZO


Thursday, March 27, 2014

Rais Jakaya Kikwete akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dk. Walter Steimeir Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo ya faragha (tete-a-tete ), huko Ikulu juzi, tarehe 25.03.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe wakipiga  picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na ujumbe aliofuatana nao wakati wakipomtembelea Rais Dkt. Kikwete, huko Ikulu juzi, tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na baadhi ya viongozi aliofuatana nao wakati walipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu juzi, tarehe 25.3.2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha wageni wake jengo la Ikulu sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani), mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo, Ikulu juzi.
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmon na  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu kwa mazungumzo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier. Waziri huyo aliwasili nchini juzi. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment