Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, John Matiko (kushoto) kuhusu Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.
Mmoja wa wanahabari ambaye ni mpiga picha wa
Televisheni ya Tumaini (katikati), akiuliza swali kwenye mkutano wa wanahabari
na kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd iliyoandaa Mkutano na Maonesho ya
Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.
Na Frank
Mvungi-MAELEZO
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano na Maonesho ya Kilimo (AGRITECH) 2014, yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es Salaam kuanzia April 10 mwaka huu na kuwashiriksha waoneshaji wa nje na ndani ya nchi katika Nyanja mbalimbali za kilimo.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa mkutano huo Dkt.Ellen
Otaru- Okoedian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa
Mikutano wa Iadara ya Habari-MAELEZO leo jijini Dara es Salaam.
Dkt Ellen amesema mkutano huo unalenga uwezeshaji
katika kilimo ambapo wakulima wa Tanzania watapata fursa ya kukutana na wadau
wakubwa wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili na kuona namna bora
ya kuinua sekta ya kilimo nchini.
Alisema mkutano huo pia utawahusisha wadau wa kilimo wakiwemo
wauzaji wa pembejeo, mbolea, na madawa ya mimea, matrekta, wanaohusika na
umwagiliaji, vyuo vya kilimo, biashara, za mazao, watafiti, Taasisi za biashara za
ndani na nje ya nchi, wakulima na wafugaji, Wizara zote husika na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Aliongeza kuwa katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza tarehe
10 hadi 12 aprili 2014 wakulima watapata fursa ya kuelewa umuhimu wa zana
bora za kilimo,utafiti , jinsi
teknolojia ya simu za mkononi inavyoweza kubadili kilimo hapa nchini.
“Mkutano huu pia utajadili fursa mbalimbali zilizopo
kwenye kilimo na mchango wa Taasisi za fedha katika kukuza kilimo hapa nchini
na washiriki watapata fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao juu ya namna bora
ya kuongeza tija katika kilimo ili kupambana na janga la njaa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla” alisema
Dk. Ellen.
Dkt. Ellen amesema mkutano huo utajumuisha washiriki
toka mataifa takribani 20 yakiwemo Ujerumani, Marekani, Ufaransa, China,
Japani, Kenya, Uganda na Malawi.
Naye Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa
Kampuni hiyo, John Matiko alitoa wito kwa wakulima hapa nchini na wadau wote wa
Sekta ya kilimo kujitokeza katika mkutano huo na pia kushiriki katika maonesho
yatakayofanyika wakati wa mkutano huo.
Kwa mujibu wa Matiko, mkutano huo utakuwa na Kaulimbiu
isemayo “Nguvu ya Teknolojia katika Mapinduzi ya Kilimo”.
No comments:
Post a Comment