Polisi watatu wanaolinda makazi ya waziri mkuu wa Pakistan wamesimamishwa kazi kwa muda baada ya Paka kumuua Tausi wa waziri mkuu.
Mtunza bustani alipata Tausi mmoja amekufa katika moja ya bustani za makazi ambapo ndege hao huvinjari , lilieleza gazeti la Express Tribune.
Maafisa 18 hawakubainika kuwa na hatia, gazeti lilieleza.Mmoja wa maafisa waliosimamishwa kazi amesema wengine 21 waliitwa kujieleza baadae. Imeripotiwa kuwa maafisa hao walisema walikuwa kazini usiku ule , lakini hawakutegemea kuwa Paka wangemla Tausi.
Lakini watatu waliosalia wote walipewa onyo na kuadhibiwa kwa uzembe
Makazi ya waziri mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif yako Raiwind, viungani mwa mji wa Lahore.
No comments:
Post a Comment