Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorious atauza nyumba yake ili aweze kumudu gharama ya kesi ya mauaji inayomkabili.
Hii ni kwa mujibu wa wakili wake Brian Webber ambaye amenukuliwa na Shirika la Wanahabari La Afrika Kusini (SAPA) akisema kesi hiyo itaendelea kwa zaidi ya wiki tatu zilizotarajiwa kwa kesi hiyo kukamilika.
Oscar hajaweza kurejea katika nyumba yake hata baada ya maafisa wa uslama kumruhusu arejee huko zaidi ya mwaka mmoja uliopita huku uamuzi ukitolewa wa nyumba ile kusalia ikiwa imefungwa hadi pale kesi hiyo itakapo kamilka.
Kwa Mujibu wa SAPA, hati za kortini zilizoandikishwa mwaka jana wakati mwanariadha huyo alipokuwa akiwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana zaonyesha kuwa nyumba hiyo iliyo katika mtaa wa Silverwoods ina thamani ya Randi millioni 5 ambazo ni sawia na dola za marekani 457 000.
Oscar anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake mnamo tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka jana huku akisema kuwa alimpiga risasi kimakosa.
Kesi ya mauaji dhidi yake ambayo kwa sasa iko katika wiki ya tatu, imehairishwa hadi siku ya jumatatu ambapo mashahidi wengine watano wa upande wa mashitaka wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kabla ya yeye kupewa fursa ya kujitetea.
Upande wa mashitaka unadai kuwa Pistorious alimpiga risasi Bi Steenkamp, aliyekuwa mwana mitindo, mtangazaji maarufu wa runinga na mwana sheria baada ya kinachodahniwa kuwa ugomvi wa nyumbani.
Huku kwa upande wake, Pistorious akisema kuwa aliamini kuwa mpenzi wake alikuwa amelala na akidhani kuwa palikuwa na mwizi nyumbani kwake alifyatua risasi kuelekea chooni asubuhi mapema mnamo tarehe 14 februari mwaka 2013.
Iwapo mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 27 atapatikana na hatia , huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha.
No comments:
Post a Comment