TANGAZO


Sunday, March 30, 2014

Skuli ya Kitope yapatiwa msaada wa madeski na NMB


 Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Kitope waliohudhuria hafla ya kupatiwa vikalio vya skuli za Donge na Kitope iliyofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Kitope.
 Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akipokea Madeski 50 kwa ajili ya skuli ya Sekondari ya Kitope kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari Khamis Mohd.
Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari Khamis Mohd akimkabidhi madeski 50 Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis kwa ajili ya Skuli ya Sekondario ya Doonge.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya NMB mara baada ya hafla ya makabidhiano ya madeski kwa ajili ya skuli za Donge na Kitope. Kushoto ya Balozi ni Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis na Mke wa Balozi Seif, Mama Asha Suleiman Iddi. Kulia ya Balozi ni Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Bwana Bakari Khamis Moha na Mwenyekiti wa Skuli ya Kitope Sekondari Nd. Ali Mussa.
(Picha zote na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ)
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
BENKI ya kuhudumia Wananchi wa Kawaida  Nchini { NMB } imekabidhi mchango wa Vikalio 100 kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika Skuli za Sekondari za Donge na Kitope zilizomo ndani ya Wilaya ya Kasakazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Msaada huo wa Vikalio wenye gharama ya shilingi za Kitanzania Milioni Kumi utasaidia kupunguza uhaba wa madeski kwa Skuli hizo za Donge na Kitope ambapo kila Skuli imefanikiwa kupata madeski 50.
 
Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar Bwana Bakari Khamis Moh’d alikabidhi  msaada huo kwa  Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis hafla iliyofanyika hapo katika skuli ya Sekondari Kitope.
 
Meneja huyo wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari aliiomba Jamii kuendelea kuiunga mkono Benki hiyo ili kusaidia kuipa nguvu za kiutendaji itakaoongeza kasi ya kusaidia harakati za Kijamii Nchini.

No comments:

Post a Comment