Ofisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, kuhusu waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi vigezo vya usaili. Kulia ni Ofisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
Ofisa habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti
ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu
waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi vigezo vya usaili. Kushoto ni Ofisa Udhibiti na Ubora wa Sekretarieti hiyo bw. Chistopher
Liganga.
Ofisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti
ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaonyesha waandishi wa
habari moja ya nakala ya maombi ya ajira isiyokidhi vigezo hali inayosababisha
waombaji wengi wenye sifa kushindwa kupata ajira Serikalini. Kulia ni Ofisa
Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi.
Frank Mvungi-Maelezo
OFISI ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma kuandaa programu ya Elimu kwa umma ili kuwawezesha waombaji wa kazi kuweza
kutimiza vigezo vinavyohitajika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi
walizooomba.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari Mkuu wa Sekretarieti ya
Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar
es salaam.
Akifafanua Bi Riziki amesema mpango huo unalenga
kuwajengea uwezo waombaji wa ajira kuweza kuandaa wasifu wao vyema (CV), kuandika
barua za maombi kwa ufasaha, kuwajengea
uezo wa kufanya maandalizi sahihi kabla ya usaili.
Aliongeza kuwa hali hiyo inatokana na kujitokeza kwa
changamoto za wahitimu walio wengi kushindwa kutimiza vigezo husika ili waweze
kupata ajira wanazoomba.
Bi Riziki alisisitiza na kusema kuwa katika kutekeleza
mpango huo watashirikiana na Taasisi za Elimu hapa nchini ili kuwasaidia
wanafunzi wanaohitimu vyuoni ili kuwajengea uwezo ili waweze kukidhi vigezo
mara wanapoomba ajira Serikalini.
Katika kipindi cha miaka mine Tangu kuanzishwa kwa
Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma imekabiliana na changamoto nyingi
ikiwemo ubora wa wahitimu wanaowasilisha maombi ya kazi Serikalini kuanzia
ngazi ya Sekondari, Astashahada ya juu, Shahada ya uzamili pamoja na shahada ya
uzamivu.
Pia Bi Riziki alibainisha kuwa katika tathmini sekretarieti
kupitia maombi ya ajira yaliyowasilishwa wamebaini mapungufu yatokanayo na
ubora hafifu wa baadhi ya wahitimu wanaoomba kazi kupitia chombo hiki.
Dhana potofu ya wahitimu kuwa kuwa na vyeti pekee
ndicho kigezo pekee cha mhitimu kupata ajira badala ya kuwa na uelewa mpana wa
kile walichoombea kazi,kutotilia maanani sifa na masharti ya Tangazo husika,
kutojiamini,kukosa uzoefu wa kazi inayohitaji uzoefu na uwezo mdogo wakutumia
lugha kwa ufasaha.
No comments:
Post a Comment