TANGAZO


Monday, March 3, 2014

Nderemo na Vifijo vyatawala kampeni za CCM Jimbo la Kalenga katika vijiji vya Msengelindete, Mahanzi Ufyambe na Uwassa


Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Msengelindete, Kata ya Uwassa, Iringa Vijijini alipowasili kufanya kampeni leo asubuhi. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio blog)
Wananchi wa Kijiji cha Msengelindete wakishangilia walipokuwa wakimlaki kijana wao, Godfrey Mgimwa ambaye amezaliwa katika Kata ya Uwassa.
Karibu mwanetu karibu mwanetu, ndivyo mama huyo wa Kijiji cha Msegelindete alivyokuwa akimlaki kwa furaha mtoto wao Godfrey Mgimwa.
 Mgimwa akiwasalimia wazee wa Kijiji cha Msengelindete.
Ni furaha iliyoje kwa akina mama kumpokea mwanao katika mkutano huo wa kampeni
Mgimwa akiwasalimia akina mama wa Kijiji cha Msengelindete.
Akina mama wakishangilia na kukubali kumpigia kura ya ndiyo Mgimwa Machi 16, mwaka huu.
Tuko tayari kumpigia kura Godfrey Mgimwa.
Katibu Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Arusha, Rehema Mohamed  ambaye alikuwa Diwani wa Chadema Arusha na kujiengua akiwaeleza wananchi ubaya wa kujiunga na Chadema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe, akinadi Godfrey Mgimwa kwa wananchi ili Machi 16, wampe kura za ndio.
Mgimwa akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Mahanzi alipowasili kupiga kampeni leo
Msanii filamu na muziki, Dokii akijiunga na wananchi kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe wakati wa kampeni za CCM, katika Kijiji cha Ufyambe Kata ya Uwassa leo.
Wananchi wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura za ndiyo Mgimwa Machi 16, mwaka huu katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Iringa, Christina Mbomela akipiga magoti mbele ya wananchi kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa  katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Ufyambe, Kata ya Uwassa, Iringa Vijijini leo.
Wafuasi wa CCM Kata ya Uwassa, wakishangilia wakati wa kumlaki Mgimwa katika mkutano wa kampeni.
Mgimwa akijinadi mbele ya wananchi katika Kata ya Uwassa.
Ni furaha iliyoje wakati wa kumlaki Mgimwa alipowasili katika mkutano wa kampeni katika Ikjiji cha Uwassa, Kata ya Uwassa.

No comments:

Post a Comment