TANGAZO


Monday, March 3, 2014

Bunge Maalum la Katiba laendelea mjini Dodoma

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Afya wa Serikali ya Zanzibar, Juma Duni Hajji (kushoto), akiwaeleza jambo wajumbe wenzake, Mawaziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui (katikati) na wa Sheria, Abubakar Khamis Bakari, wote wa serikali hiyo, kwenye viwanja vya Bunge, baada ya kuaghirishwa kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe kutoka Zanzibar, Waziri wa Fedha wa Serikali ya Zanzibar, Omar Yussuf Mzee (kushoto) na Hamad Masoud Hamad, wakielekea kwenye ukumbi wa bunge.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Profesa Mark Mwandosya, akifurahia jambo na mjumbe mwenzake, Mary Nagu, wakati walipokuwa wakielekea kwenye ukumbi wa bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta (kushoto) na Kingunge Ngombale Mwiru, wakizungumza jambo ndani ya bunge hilo. 
Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha bunge hilo kilichofanyika leo.
Mjumbe wa bunge hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Lipumba (kushoto), akichangia mada wakati wa kikao hicho kuhusu marekebisho ya Rasimu ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akipitia nakala ya marekebisho ya Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, wakati wa kikao hicho.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimweleza jambo mjumbe mwenzake, Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, ndani ya ukumbi wa bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ole Sendeka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kwenye viwanja vya Bunge, mara baada ya kuaghirishwa kikao cha bunge hilo leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, kwenye viwanja vya Bunge leo.
Mjumbe wa bunge hilo, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (wa pili kushoto), akizungumza jambo na wajumbe wenzake, kwenye viwanja vya bunge leo. 

No comments:

Post a Comment