Shughuli ya kutafuta ndege ya
abiria ya Malaysia imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya
suitofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea
wakiwa katika ndege hiyo.
Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza
mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa
imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege
hiyo.Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.
No comments:
Post a Comment