* Wengi wamlalamikia Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutokana na alivyoiteua Kamati ya Uongozi
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki (kulia), akimueleza jambo mjumbe mwenzake, Amina Makilagi, wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka Zanzibar, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge tayari kwa kikao, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifurahia jambo kwenye viwanja vya Bunge, wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge tayari kwa kikao cha asubuhi, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika, akizungumza, wakati alipokuwa akilalamikia uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, uliofanywa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta. Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akizungumza, wakati alipokuwa akijibu baadhi ya shutuma za kuteua wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa kile kilichodaiwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo, kuwa ni kwa upendeleo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Habibu Mnyaa (chini kushoto), akitaka muongozo kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, kwa kile alichodai uwiano usio sawa kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa upande wa Zanzibar, wakati wa kikao hicho leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza wakati alipokataa uteuzi wa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya uongozi kwa madai ya kukiukwa uteuzi wa kamati hiyo na kutoa upendeleo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha CHAUSTA, James Mapalala, akilalamikia Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kamati namba moja, ambayo yeye ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka kundi la watu wenye ulemavu, Vicent Mzena, akimlalamikia Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta kwamba asiwe akiwateua wajumbe wale kila inapotokea kuundwa kamati za mambo mbalimbali na badala yake, ateue wajumbe wengine katika kundi hilo kwa kuwa kuna walemavu wa makundi mbalimbali.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, David Kafulila, akimsihi Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, kuwa awe akitumia busara anapoteua wajumbe wa Kamati ya uongozi na aache kupendelea chama ama kundi fulani.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ave-Maria Semakafu, akizungumzia suala la uteuzi huo na kudai suala hilo lilikosewa tokea hatua za mwanzo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kangi Lugora, akimsihi Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta kufanya uadilifu kwa kuwaingiza wajumbe wengi kutoka upinzani ili kuleta muonekano wa Kitaifa katika suala la kuunda Katiba mpya.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia akimsihi Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta kuwa wajumbe wa bunge hilo, waweke utaifa mbele kwa ajili ya kufanikisha upatikanaji wa Katiba mpya iliyo nzuri na kuacha kuweka mbele masuala ya vyama vyao.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) na wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia), wakizungumza jambo na mjumbe mwenzao, Kingunge Ngombale Mwiru, kwenye viwanja vya Bunge, baada ya kuaghirishwa bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohammed Said Mohammed (kulia), akisalimiana na mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo jana. Katikati ni mjumbe mwenzao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
No comments:
Post a Comment