TANGAZO


Saturday, March 29, 2014

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aungana na Wananchi katika kuuaga Mwili wa John Tuppa mjini Dodoma

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akiongoza mamia ya wananchi pamoja na viongozi wa Serikali, Siasa na Dini wa Mji wa Dodoma na Vitongoji vyake katika kuuaga mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, marehemu John Tuppa, mjini Dodoma jana. Nyuma yake Balozi Seif alifuatiwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda.
Mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gariel Tuppa aliyefariki Dunia Juzi Tarehe 26/3/2014, ukiingizwa ndani ya Bunstani ya Nyerere Square kati kati ya Vitongoji wa Mji wa Dodoma kwa ajili ya Ibada Maalum ya Kuuaga jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Pili kutoka Kulia akiwaongoza Mamia ya wakaazi wa Mji wa Dodoma katika kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gariel Tuppa ndani ya Viunga vya Nyerere Square Mjini Dodoma. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na Spika wa Bunge la Muungano Mh. Anna Makinda na kushoto yake Balozi Seif, ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Mke wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, marehemu John Gariel Tuppa Mama Tupa Gabriel (wa pili kulia) pamoja na wana familia ya marehemu wakiwa kwenye Misa ya kuuaga mwili wa marehemu mumewe, ndani ya Bustani ya Nyerere Squre, Mjini Dodoma jana.
Wana Kwaya ya Mtakatifu Sifiria chini ya muongozaji wao, Francis Patrick wakiendelea na nyimbo za Ibada katika Misa ya kuuaga mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, marehemu John Gariel Tuppa. (Picha zote na Hassan Issa OMPR)


Na Othman Khamis, OMPR
Mamia ya wananchi na Wakaazi wa Mji wa Dodoma na vitongoji  vyake jana wameuaga rasmi mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tuppa aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Marehemu John Gariel Tuppa alilazimika  kupatiwa huduma za matibabu baada ya kuugua ghafla ugonjwa  wa Shindikizo la Damu { Blood Pressure } akiwa katika Vikao vya kazi  Wilayani Tarime.

Misa ya kumuombea Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara iliyoongozwa na Makamu Askofu wa Kanisa Katoliki la Mkoa wa Dodoma Father Chesco Msaga ilifanyika katika Uwanja wa Nyerere Suare kati kati ya Vitongoji vya Makao Makuu ya Serikali Mjini Dodoma.

Wakiwa katika hali ya majozi mamia  ya wananchi hao wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, Mawaziri wa Serikali zote mbili, Viongozi wa Dini tofauti wakiwemo pia wawakilishi wa mashirika na Taasisi za Kimataifa walipata fursa ya kuuaga mwili wa Maheremu John Gabriel Tuppa.

Wakiwasilisha salamu mbali mbali wawakilishi wa Serikali, Viongozi wa Dini na Taasisi tofauti za Kijamii walimueleza Marehemu John Gabriel Tuppa kwamba ni Kiongozi wa mfano atakayekumbukwa miaka kadhaa ijayo kutokana na mchango wake hasa katika masuala ya Kijamii.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mh. William Lukuvi alisema miaka 20 ya Utumishi wa Marehemu John Gariel Tuppa ndani ya Manispaa ya Makao Makuu Mjini Dodoma (CDA) utaendelea kukumbukwa na wananchi walio wengi Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment