Mfuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Coletha Mitao akitafakari jambo alipokuwa akimsikiliza
mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa wakati wa
kampeni za uchaguzi katika Kijiji cha Muwimbi, Kata ya Lumuli, Iringa
Vijijini leo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia CCM, Godfrey Mgimwa, akisalimiana na akinamama wa Kijiji cha Mfukulenge, Kata ya Ifunda, Iringa Vijijini leo, baada ya mkutano wa kampeni kumalizika. |
Akinamama wakimsikiliza kwa makini Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, alipokuwa akitoa somo la upigaji kura katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Muwimbi, Kata ya Lumuli, Iringa Vijijini leo. Meneja wa Kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Meja mstaafu Mbuta akielezea umuhimu wa kumchagua Godfrey Mgimwa katika uchaguzi utakaofanyika Jumapili Machi 16, mwaka huu. Akinamama wakipiga makofi baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Mfukulenge, Kata ya Ifunda leo. Mgimwa akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Mfukulenge baada ya kumalizika mkutano wa kampeni leo. Wananchi wa Kijiji cha Mfukulenge, wakisalimiana na mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa baada ya mkutano wa kampeni kumalizika leo. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)
No comments:
Post a Comment