*Aiasa Jumuiya kujipambanua
*Asema lazima iwe na kitu cha kujivunia
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo, Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma leo, alipofika kwa ajili ya kuifungua Semina Elekezi kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), akielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM, baada ya kuangalia na kusikiliza kwaya ya Kambarage, kwa ajili ya kwenda kuifungua Semina Elekezi kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho, Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto), akielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya Makao Makuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuangalia na kusikiliza kwaya ya Kambarage, kwenda kuifungua Semina Elekezi kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho, Mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa semina hiyo, wakimshangilia Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akiingia kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kuifungua semina elekezi kwa viongozi hao leo.
Wajumbe wa Semina hiyo, wakicheza baada ya Waziri Mkuu kuingia kwenye ukumbi wa CCM kwa ajili ya kuifungua semina hiyo leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Wazazi wakipiga makofi baada ya kuingia kwenye ukumbi huo kwa ajili ya kuifungua semina hiyo elekezi kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za Jumuiya hiyo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa semina, wakiimba na kucheza, mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jumuiya hiyo, wakiangalia makabrasha yao.
Wajumbe wakisikiliza shairi lililokuwa likisomwa na mmoja wa wajumbe kutoka Zanzibar, Farida Rajab Taufik, wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), akimwangalia msoma shairi wakati alipofika kufungua semina hiyo elekezi. Kusoto ni Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaj Abdallah Bulembo na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dogo Idd Mabrouk.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dogo Idd Mabrouk.
Waziri Mkuu akiimba wimbo wa Kwaya ya Kambarage pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi, Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto) na Makamu wa jumuiya hiyo, Dogo Idd Mabrouk.
Wasanii wa Kwaya ya Kambarage, wakitumbuiza katika ufunguzi wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuifungua rasmi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaj Abdallah Bulembo, akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuifungua rasmi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisikiliza na kutafakari hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dogo Idd Mambrouk.
Wajumbe wakisiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wao wa Jumuiya, Alhaj Abdallah Bulembo wakati wa ufunguzi wa semina yao hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa hotuba yake, wakati alipokuwa akiifungua Semina Elekezi ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za jumuiya hiyo, Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa hotuba yake, wakati akiifungua Semina Elekezi ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za jumuiya hiyo, Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifafanua jambo, wakati alipokuwa akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Semina Elekezi ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM, kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za jumuiya hiyo, Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu akifafanua jambo wakati akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa semina hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dogo Idd Mabrouk (wa tatu) na Katibu wa Organizesheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Seif Khatib, wakiimba mara baada ya kuifungua semina hiyo ya Jumuiya ya Wazazi, mjini Dodoma leo.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dogo Idd Mabrouk, akitoa shukurani za Jumuiya kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mara baada ya kuifungua semina hiyo leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia), akimkabidhi seti ya jezi mmoja wa Wakuu wa Shule za Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nelson Kangero wa Shule ya Sekondari ya Lomwe, mkoani Kilimanjaro, wakati alipofungua Semina Elekezi kwa viongozi wa Mikoa, Wilaya pamoja na Wakuu wa Shule za jumuiya hiyo, Mjini Dodoma leo.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Jumuiya ya Wazazi
nchini ni miongoni mwa jumuiya inayoongoza na kusimamia masuala yote yanayohusu
elimu, malezi bora kwa vijana wa taifa letu hivyo lazima iangalie jinsi ya
kuweza kujipambanua katika utekelezaji wa Umoja wa Jumuiya yao.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Februari
22, 2014), wakati akifungua rasmi semina ya siku tatu ya viongozi na watendaji
wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya Tanzania
inayofanyika kwenye Ukumbi wa NEC, Mkoani Dodoma.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu Pinda
aliwaeleza wana jumuiya hao kuangalia malengo wanayojipangia aidha yawe
ya muda mfupi au mrefu ili kuyatekeleza kwa kuzingatia yale mambo ya msingi na
yenye kipao mbele kwa wananchi.
“Changamoto kubwa iliyopo mbele yenu kama viongozi na
watendaji wakuu wa Jumuiya hii ni namna ya kutimiza malengo mliyojiwekea“.
Alisema, dhana ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi nchini ni
kuongeza na kuboresha masuala yote yanayohusu Sekta ya elimu hapa nchini:
‘‘Tumieni semina hii kujipima kwamba mmefikia wapi katika utelelezaji wa
malengo yenu kwa kuangalia mapungufu na maboresho katika jumuiya yenu‘‘.
Jumuiya ya Wazazi ndio magwiji mnaoongoza kwa kuwa na
shule nyingi hapa nchini, hivyo jumuiya yenu ijipange na kusimamia vema shule hizo
ili kuwa vinara katika kuboresha masuala ya elimu hapa nchini. Akitoa mfano,
alisema: “Kwanini shule za binafsi zinakuwa zinaongoza kuliko shule zilizopo
ndani ya Jumuiya yenu, walau katika kumi bora iwepo shule moja kutoka Jumuiya
ya Umoja wa Wazazi alisema Waziri Mkuu”.
Kutokana na kauli hiyo, Waziri Mkuu aliiambia Jumuiya
hiyo kutumia dhana ya elimu kama ngao yao katika kuleta maendeleo katika Sekta
hiyo kwani Ilani ya chama cha Mapinduzi imetamka wazi kuongeza kasi ya upanuzi
wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari lengo ambalo ni moja ya jukumu kuu la
msingi la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi.
Aliendelea kusema kuwa Jumuiya ya Wazazi inajukumu la
kusimamia masuala yote yanayohusu maadili, jukumu ambalo halina tofauti sana na
jukumu la madhehebu ya dini kuzungumza bayana masuala ya malezi ya watoto na
vijana ambayo yamekuwa yakiporomoka kila kukicha, hivyo Waziri Mkuu alisema, jumuiya
hii itumia jukumu na nafasi waliyopewa kuhakikisha watoto wote walio ndani na
nje ya jumuiya wanafundishwa maadili.
Waziri Mkuu aliendelea kusema kuwa, Jumuiya ya Umoja wa
Wazazi ina majengo, viwanja na ardhi inayofaa kwa kilimo na shughuli za
kiuchumi, tumieni fursa hizi kwa kujenga vyuo, kuanzisha miradi ya maendeleo
ambayo itawasaidia katika kuongeza kipato katika jumuiya yenu.‘‘Mnachotakiwa ni
kupanga bajeti zenu vizuri na kusimaia utekelezaji pamoja kusimamia vizuri
miradi na fursa zinazojitokea“
Pamoja na hayo, Waziri Mkuu aliiomba Jumuiya ya Wazazi
kujitokeza kuzungumzia masuala ya Dawa za Kulevya kwa kusema kuwa, wako vijana
ambao wametumbukia katika dimbwi la Dawa za Kulevya ambaa pia wanahatarisha
maisha yao kwa kupata UKIMWI: “Ni matumaini yangu kwamba Jumuiya ya Umoja wa Wazazi
itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii, kutoa ushauri kwa vijana kuhusu
athari za dawa za kulevya, UKIMWI na
hata mkiweza kuanzisha vituo vya ushauri”, alisisitiza Waziri Mkuu.
“Ili kuweza kuwa na Jumuiya ya Wazazi imara ni dhahiri
kuwa wanajumuiya wasimamie kanuni na maadili yanayoongoza jumuiya yao kwa
kuwaasa kuacha kujiingaza katika makundi yasiyokuwa na msingi hasa kwa
kutanguliza maslahi ya fedha katika kupata nafasi za uongozi katika kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi mkuu ambao huleta migawanyiko kati ya Viongozi na
wanachama na wapiga kura”. Mzingatie masuala yanayohusu kujenga na kukuza
utekelezaji wa jumuiya yenu ambayo itawasaidia kujenga jumuiya imara na kujenga
chama imara kitakacho leta viongozi imara”alisisitiza Waziri Mkuu.
Mapema,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa, Bw. Majura Bulembo, alisema
lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo na kuwaongeza ufanisi Jumuiya ya
Wazazi katika utekelezaji kazi zao na
kuwasisitiza kuhudhuria semina hiyo ipasavyo ili kuweza kukumbusha mapungufu na
changamoto zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
“Viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi za uongozi
walizopewa kwa kujiona wao ndio viongozi wakuu kwa kujifanyia maamuzi yao,
viongozi kama hao wataondolewa madarakani mara moja”.
No comments:
Post a Comment