Mahakama moja ya Misri imewahukumia kifo watu 26 kwa makosa ya kuanzisha mtandao wa ugaidi uliopanga mashambulizi dhidi ya meli zilizopitia kwenye kito cha Suez.
26 hao pia walipatikana na makosa ya kuunda mabomu, pamoja na kuchochea ghasia na mashambulizi dhidi ya jeshi na waumini wa Kikristo.
Wote walihukumiwa bila kuwepo mahakamani. Hukumu hiyo sasa inasubiri kuidhinishwa na afisa wajuu wa Kiisilamu. Katika miezi ya karibuni Misri imeshuhudia mashambulio ya kuvizia yanayolaumiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Kiisilamu.
No comments:
Post a Comment