TANGAZO


Monday, February 24, 2014

Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuaghirishwa leo

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaghirishwa kwa kikao cha kujadili kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Profesa Juma Kapuya (kushoto) na Haroub Mohamed Shamis, wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaghirishwa kikao cha kujadili kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Juma Maalim na Namelok Sokoine wakizungumza nje ya ukumbi huo leo, mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Shamim Khan (kushoto), akimweleza jambo, mjumbe mwenzake, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaghirishwa leo. Kulia ni mjumbe Richard Ndasa.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Vita Kawawa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuaghirishwa kikao hicho, nje ya ukumbi wa Bunge leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ibrahim Muhamada Sanya (kushoto), akizungumza jambo na wajumbe wenzake,Vita Kawawa, Ismail Jusa Ladhu na Margreth Sitta, nje ya ukumbi wa bunge leo. 

No comments:

Post a Comment