Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu katika Tafrija Maalum ya kukaribishwa kwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma jana.
Waziri Mkuu Mizengo Pind, akitoa hotuba yake kwenye Tafrija Maalum ya kukaribishwa kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Mlimani Grand Mark, Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza Wabunge, Wawakilishi na wabunge wa Bunge la Katiba kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Tafrija Maalum ya kukaribishwa Wabunge hao, Mjini Dodoma jana. Nyuma yake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Salum Turky na Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Shamsi Vuai Nahodha, wkichukua chakula kwenye tafrija maalum ya kukaribishwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mjini Dodomajana.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mwamboya pamoja na Mwakilishi wa Viti Maalum, Salma Bilal wakijumuika na waheshima wenzao, wakijipatia chakula kwenye Tafrija maalum ndani ya Ukumbi wa Mlimani Grand Mark, Mjini Dodoma jana.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akiwa sambamba na Waziri wa Nchio Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi wakivaa koti saizi ya miili yao kwenye Tafrija la Kukaribishwa kwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma jana.
No comments:
Post a Comment