TANGAZO


Sunday, February 2, 2014

Vurugu uchaguzi wa Thailand ukianza

 


Maelfu ya wapinzani wametatiza shughuli ya kupiga kura wakipinga serikali
Waziri mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra amepiga kura katika uchaguzi mkuu unaoendelea ncini humo huku ilinzi ukiwa umedhibitiwa vikali.
Uchaguzi huu unafanyika baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya wapinzani kujaribu kutatiza hali ili usifanyike.
 
Upinzani rasmi, unasusia uchaguzi ukitaka badala ya uchaguzi, kuundwe kamati itakayochukua nafasi ya serikali ili kupambana na ufisadi.
Mwandishi wa BBC mjini Bangkok anasema kuwa waandamanaji, wanawazuia wapiga kura kupiga kura na pia kuzuia karatasi za kupigia kura kufikishwa katika vituo vya kupigia kura.
Lakini katika maeneo mengine, shughuli ya kupiga kura inaendelea bila matatizo yoyote.
Katika mtaa mmoja shughuli ya kupiga kura imesitishwa kabisa baada ya tukio la ufyatulianaji risasi kati ya wapinzani na wafuasi wa serikali.
Wapinzani wanadai kuwa serikali inategmea sana ufisadi kusalia madarakani.

No comments:

Post a Comment