TANGAZO


Sunday, February 2, 2014

Kikosi cha AU chakomboa mji CAR

 

Wanajeshi wa Ufaransa wakiwakamata wapiganaji wa Seleka Bangui
Kamanda wa kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema askari wake wameukomboa mji wa Sibut, kutoka kwa wapiganaji wa zamani wa Seleka.
Kamanda huyo, Jenerali Tumenta Chomud, alisema askari kutoka Gabon sasa wako mjini Sibut, na watawanyang'anya silaha wapiganaji waliouteka mji huo Alkhamisi.
Wapiganaji wa zamani wa Seleka - wengi wao Waislamu - wamekuwa wakiondoka mji mkuu, Bangui, ambao uko kama kilomita 200 kusini ya Sibut.
Kuondoka kwa Seleka kumezusha mauaji ya kulipiza kisasi, na watu zaidi ya 40 wameuwawa mjini Bangui katika siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment