TANGAZO

Friday, February 28, 2014

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), waanzishwa mjini Dodoma

VIONGOZI wa Vyama, Taasisi na watu wenye malengo yanayofanana, wameanzisha Umoja utakaosimamia kupatikana Katiba ya Wananchi (UKAWA), mjini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye yuko katika Umoja wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa umoja wao huo, unaamini kuwa Rasimu ya Kanuni itakayotumika katika kuendesha vikao vya bunge hilo, kuwa ndio roho ya kuongoza mjadala wa rasimu ya katiba wanayoitunga.

Umoja huo, kwa mujibu wa viongozi wake wa muda, wajumbe wake watakuwa wakitetea Rasimu ya Katiba kama ilivyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwa tayari kuiboresha kwa kuzingatia maoni ya wananchi bila kile walichokiita kuichakachua kutokana na misimamo ya taasisi ama makundi yao.

Profesa Lipumba alisema kuwa kama kanuni hizo zisipokuwa nzuri basi hata hiyo Katiba nayo haiwezi kuwa nzuri, kwani haitoweza kukidhi matakwa ya wananchi.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, kuhusu umoja wao wa Utetezi wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambao utakuwa ukitetea Rasimu ya Katiba kama ilivyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na pia kuwa tayari kuiboresha kwa kuzingatia maoni ya wananchi bila kile walichokiita kuchakachuliwa. Kushoto ni wajumbe wenzake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Eng. Pamela Maassay. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni mjumbe wa bunge hilo, Profesa Abdallah Safari.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, kuhusu umoja wao wa Utetezi wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ambao utakuwa ukitetea Rasimu ya Katiba kama ilivyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari alipokuwa akijibu maswali katika mkutano huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Profesa Abdallah Safari (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari alipokuwa akijibu maswali katika mkutano huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Eng. Pamela Maassay, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment