Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala (kushoto) akimuuliza swali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo aliyekaa kulia, wakati alipokuwa akifanya nae mahojiano juu ya kazi zifanywazo na Bodi ya Filamu ikiwemo kufungia na kuruhusu filamu nchini.
Mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala (kushoto) akimuuliza swali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo aliyekaa kulia, wakati alipokuwa akifanya nae mahojiano juu ya kazi zifanywazo na Bodi ya Filamu ikiwemo kufungia na kuruhusu filamu nchini.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akijibu swali toka kwa mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala (kushoto) wakati wa mahojiano na Katibu huyo jana jijini Dar es Salaam.
Mjumbe toka Bodi ya Filamu, Bi. Beatrice Sumari akifuatilia kwa makini mahojiano kati Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania na mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala yaliyofanyika leo ofisi za Bodi ya Filamu jijini Dar es Salaam jana.
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza jambo
wakati alipokutana na mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana.
Pancras Mayala (kushoto) leo katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam.
Na Benedict Liwenga-Maelezo
BODI ya Filamu nchini imekiri ongezeko la uzingatiaji wa Sheria ya Filamu na kanuni
zake unaofanywa na watengenezaji na wasambazji wa filamu wa ndani na nje ya
nchi.
Aidha imethibisha kuwa uwasilishaji wa filamu kwenye Bodi umeongezeka kwa
kiwango cha kuridhisha baada ya wengi wa wadau kuitikia wito wa kuwasilisha
kazi zao ili ziweze kukaguliwa na kupewa madaraja stahiki.
Vile
vile Bodi imefafanua kuwa filamu na muziki
iliyo katika video isiyofungiwa kwa kukosa maadili na zinazoendelea
kurushwa ama kuonyeshwa bila kuzuiwa haimaaninishi ni halali isipokuwa zinapaswa
kuwasilishwa Bodi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kabla ya kwenda kwa walaji.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo
wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds Media Group ofisi kwake jijini
Dar es Salaam.
Bi.
Fissoo amesema kuwa Bodi ya Filamu ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Filamu
na Michezo ya Kuigiza namba 4 ya mwaka 1976 Sheria ambayo ilitanguliwa na
Sheria ya Picha za Sinema ya mwaka 1930 jambo linalodhihirisha ukongwe wa
tasnia ya filamu nchini. Bodi inafanya kazi zake kwa kujielekeza katika
kusimamia Sheria hiyo na kanuni zake.
Akijibu
swali toka kwa mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana Pancras
Mayala, lililotaka kujua filamu ngapi zilizofungiwa na Bodi ya Filamu na sababu
za kufungiwa kwa filamu hizo, Bi. Fissoo amesema kuwa mpaka sasa Ofisi yake
imepoke na kushughulikia jumla ya kazi zipatazo 1059 kutanzia 2011 hadi Januari
2014 ikiwa ni kwa maana ya majina.
“Mwaka
2011 mpaka sasa tumepokea na kushughulikia filamu 1059, ikiwa ni kwa maana ya
majina, lakini ukienda kwa maana ya Part 1 na Part 2 maana yake ni jumla ya filamu
2118 ambapo kati ya hizo filamu 123 sawa na asilimia 5.8 zilielekezwa kufanyiwa
marekebisho na filamu 7, sawa asilimia 0.33 hazikuruhusiwa kati ya mwaka 2011
hadi juni 2013, ambazo ni za ndani na za nje 2.4 hazikuruhusiwa.
Aidha, kati ya
Julai 2013 hadi 2014, jumla 570 zilipokelewa zikiwemo filamu 263 zilizokuwa
zimeshaingia sokoni na kati ya hizo filamu 16 zilielekezwa kufanyiwa
marekebisho.
Tayari filamu zilizoelekezwa kufanyiwa marekesho, 14 zimekwisha
wasilishwa na kupewa kibali na filamu mbili za MV Spice na Nimekubali Kuolewa
hatujapokea marekebsho. Hakuna filamu iliyofungiwa kati ya julai 2013 hadi
Januari 2014”, alisema Bi. Fissoo.
Aliwapongeza wadau wa filamu kwa kupunguza kwa
kiasi kikubwa filamu zisizoendana na maadili na kusisitiza umuhimu wa
kuzingatia ubora na viwango.
Kwa
upande wake mtangazaji wa Clouds Media, Bwana Mayala alitaka kujua ni vigezo
gani vinavyotumika katika kuzuia filamu zisiende kwa watumiaji ambao ni
watazamaji, Bi. Fissoo alifafanua kuwa Bodi ya Filamu inazuia filamu kwa mujibu
wa sheria na vipo vipengele mbalimbali vitumikavyo katika kufanya zoezi hilo, aidha alimpitisha mtangazaji huyo katika vifungu hivyo vya sheria na kanuni, vile vile alieleza kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo, maneneo yote yanayoshauriwa
kurekebishwa au kuondoshwa hupitiwa kwa pamoja kati ya Bodi na wenyekazi na
kufikia muafaka.
"Katika eneo hilo tumeendelea kupata ushirikiano mkubwa sana", alisema Bi. Fissoo.
Aidha,
Bi. Fissoo amewaasa wadau mbalimbali wa filamu Tanzania kushirikiana kwa pamoja
katika kutekeleza mambo yaliyoelekezwa kwa mujibu wa sheria, na kwa wasanii
amewasisitizia kuwasilisha miswada ya kazi zao ili iweze kupitiwa na Bodi na
baadae filamu iwezwe kutengenezwa. Alisisitiza kuwa ofisi za Bodi ziko wazi kwa
wadau wote na wakati wowote wanapohitaji ufafanuzi wanakaribishwa kwa bodi kwa ajili
ya kuwahudumia wananchi wote
No comments:
Post a Comment