TANGAZO


Sunday, February 9, 2014

TAHA yapata Mwenyekiti mpya

Mwenyekiti mpya wa TAHA, Bw. Eric Ng'imaryo, akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Na Mwandishi Wetu
TAASISI inayoshughulika na kilimo cha maua na mboga mboga nchini (TAHA) imemteua Bw. Eric Ng'imaryo kama Mwenyekiti wake mpya kuchukua nafasi iliyoaachwa wazi na Bw. Colman Ngalo, ambaye ameiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio kwa takribani miaka kumi ya utawala wake.

Sambamba na uteuzi huo pia Bw. Ng'imaryo, pia taasisi hiyo ilimpata Makamu Mwenyekiti mpya pamoja na wajumbe nane wa Bodi ya TAHA pia walichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa TAHA (AGM) uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Miongoni mwa wanaounda Bodi mpya ya taasisi ya TAHA ni pamoja na: Bi. Fatma Riyami, Bw. Ravi Bhalerao, Bw. Herald Peeters , Bw. Juma Lossini, Bw. Robert Daniel, Bw. Tjerk Scheltema na Bw. Adrian Moss. 


Bw. Juma Ally Juma amechaguliwa kama mwakilishi kwenye taasisi ya Bodi ya TAHA kutoka jimbo la uchaguzi Zanzibar.


Taasisi hiyo ya TAHA kwa sasa imekuwa ikikuza msendeleo ya wakulima nchini ambayo hatua inayoonesha kujitolea katika kukuza maendeleo ya sekta ya maua na mboga mboga nchini.

Kablya ya uteuzi huo, Bw. Ng'imaryo alikuwa Mwenyekiti wa Arusha Blooms Company Limited, kampuni ambayo ni mwanachama wa TAHA na moja ya wazalishaji wakubwa wa mboga mboga nje ya nchi na nchini. 


Bw. Ng'maryo kitaalamu ni mwanasheria ambaye amekuwa akifanya kazi zake za kisheria katika Tanzania tangu mwaka 1987. Hata hivyo, Mwnyekiti huyo mpya ni mfanyabiashara, mkulima na mwandishi mahiri.

"Nimepata heshima kubwa na ya kipekee kabisa kuweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TAHA na niuangalia uteuzi huu kutekeleza wajibu na majukumu kwa kufanya kazi na Bodi na Sekretarieti ili kuhakikisha kwamba dira yetu inatekelezwa. 


Nami nitakuwa sehemu ya kuifanya taasisi yetu ya TAHA kuwa na mafanikio zaidi katika siku zijazo.


Ninapenda pia kuwashukuru Bw. Colman Ngalo, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, kwa uongozi wake mzuri.

Bw. Ngalo amekuwa nguzo ya TAHA kwa miaka kumi iliyopita. 


Bw. Ng'imaryo pia alitoa shukrani zaidi kwa Bi. Jacqueline Mkindi,
Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, samabmba na Sekretarieti nzima ya TAHA kwa mchango wao mkubwa kwa taasisi na sekta nzima ya maua na mboga mboga. 


"Jacqueline amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mfano. Utendaji wake wa kazi umeijenga taasisi yetu uaminifu na heshima kutoka kwa Serikali na Washirika wa Maendeleo."

Katika hotuba yake, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Bw. Ngalo ameusifu uamuzi wa TAHA wa kuweza kumchagua Bw. Ng'imaryo ambapo ameleelezea kuwa na imani na uongozi wake ambao utaleta mageuzi ya kweli kwenye sekta ya maua na mboga mboga. 


"Kwa niaba ya Bodi ya TAHA inayomaliza muda wake, napenda kumpongeza Bw. Eric kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAHA na ni mategemeo yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi pamoja naye katika miaka ijayo.

Mchanganyiko wa ujuzi wake katika sekta ya maua na mboga mboga na uzoefu mkubwa sambamba na utaalamu unafanya kuwa mtu bora kuchukua nafasi ya Uenyekiti wa TAHA na sekta yenye maendeleo endelevu. 


"Napenda pia kuishukuru Sekretarieti ya TAHA na wanachama wake kwa ushirikiano wao bora katika muongo uliopita. Kwa ushirikiano tumepata mafanikio mkubwa. Mimi ninajisikia fahari kubwa kukabidhi taasisi hii yenye mafanikio ambayo bado ina fursa kubwa kwa ukuaji zaidi katika TAHA na sekta nzima kwa ujumla."

TAHA ni taasisi ambayo ni mwanachama wa sekta binafsi ambapo imekuwa ikishiriki kwa ufanisi katika kubadilisha kilimo cha sekta ya maua na mboga mboga toka kuanzishwa kwake mwaka 2004.

Kutokana wa hatua za uwepo wa TAHA , sekta ya maua na mboga mboga nchini na kufanikiwa kuvutia washirika mbali mbali kutoa misaada mikubwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania na Washirika kama vile USAID, BEST- AC, Ubalozi wa Uholanzi , ITC, na Serikali Finland.

TAHA inatoa sapoti mbali mbali kwa wadau wa sekta ya maua na mboga mboga ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye majukwaa, kulinda na kukuza maslahi ya watendaji katika sekta hiyo ya maua yaani wazalishaji, wauzaji, wasindikaji, na watoa huduma ya maua, matunda , mboga, viungo, mimea na mbegu za maua.

No comments:

Post a Comment