Thomas Mkude, Ramadhan Singano 'Messi', na Issa Rashid 'Baba Ubaya', wote wa Simba, wakishangilia bao hilo, dhidi ya Oljoro JKT FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Thomas Mkude, Ramadhan Singano 'Messi', na Issa Rashid 'Baba Ubaya', wakishangilia bao hilo, dhidi ya Oljoro JKT FC.
Thomas Mkude na Awadh Juma, wakishangilia bao hilo, dhidi ya Oljoro JKT FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akijaribu kumtoka Aziz Yussuf wa Oljoro JKT, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo, uwanjani hapo leo.
Golipa wa Oljoro JKT, akiruka kuudaka mpira ulioelekezwa langoni kwake.
Amisi Tambwe wa Simba akipambana na Aziz Yussuf wa Oljoro JKT.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba akiwania kuudhibiti mpira wa juu huku akifuatwa Aziz Yussuf (nyuma) na Ali Omar wote wa Oljoro JKT.
Haruna Chanongo wa Simba akijaribu kumtoka Ali Omar wa Oljoro JKT.
Ramadhan Singano wa Simba (kushoto), akijaribu kumpiga chenga, Aziz Yussuf wa Oljoro JKT.
William Lucian wa Simba akipambana na Majaliwa Mbaga wa Oljoro JKT.
Donald Mosoti wa Simba akiruka juu kuwania mpira na Ali Omar wa Oljoro JKT.
Ali Omar, akiondoa hatari langoni kwake huku akifuatwa na Haruna Chanongo wa Simba.
Golikipa wa Oljoro JKT, akiudaka mpira huku akipambana na wachezaji wa Simba, wakati wa purukushani kwenye lago lake.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba akikimbilia mpira na Aziz Yussuf wa Oljoro JKT.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akipambana na Aziz Yussuf wa Oljoro JKT, wakati timu zao zipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Aziz Yussuf wa Oljoro JKT, akiondoa mpira kwa kichwa huku akizongwa na Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akimtoka Aziz Yussuf wa Oljoro JKT katika mchezo huo.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akiwania mpira na Aziz Yussuf wa Oljoro JKT.
Hili lilikuwa ni bao la pili lililofungwa na Amisi Tambwe.
Amisi Tambwe akisujudu na mwenzake Ali Badru, baada ya kufunga bao hilo la pili katika mchezo huo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao hilo la pili kwa timu yao hiyo.
Issa Rashid 'Baba Ubaya', akimpongeza Ramadhan Singano baada ya kutoa pasi kwa Amisi Tambwe aliyefunga bao hilo kwa timu yao ya Simba.
Hadi wakati huo, ubao wa matangazo ulikuwa ukionesha Simba mabao 2 Oljoro JKT 0.
Amisi Tambwe wa Simba akipambana na golikipa wa Oljoro JKT, Mohamed Ali huku Aziz Yussuf wa timu hiyo akiangalia.
Amis Tambwe wa Simba akiwania mpira na Nurdin Mohamedwa Oljoro JKT.
Amisi Tambwe wa Simba, akifunga bao la tatu kwa timu yake hiyo, huku golikipa wa Oljoro JKT FC, Mohamed Ali na Nahodha wake, Nurdin Mohamed wakiangalia mpira unavyoingia wavuni.
Amisi Tambwe, Amri Kiemba na Issa Rashid wakishangilia bao hilo la tatu kwa timu yao hiyo dhidi ya Oljoro JKT FC.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba, akimtoka Aziz Yussuf wa Oljoro JKT, wakati timu zao zipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Haruna Chanongo wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Ali Omar wa Oljoro JKT FC.
Mwamuzi wa mchezo kati ya Simba na Oljoro JKT FC, Nathan Lazaro, akimkabidhi mpira Amisi Tambwe wa Simba, baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika mchezo huo, wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba ilishinda mabao 4-0.
Amisi Tambwe wa Simba, akikabidhiwa mpira wake na mwamuzi Nathan Lazaro, mara baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika mchezo huo.

No comments:
Post a Comment