TANGAZO


Saturday, February 1, 2014

Khadija Kopa awapeleka puta mashabiki wa Taraab Mbeya


Malkia wa Taarab nchini, Bi. Khadija Kopa akiimba mbele ya umati wa watu kwenye ukumbi maarufu wa City Pub, usiku wa kuamkia leo, jijini Mbeya. Malkia huyo aliwapelekesha mashabiki wa faini hiyo kwa nyimbo zake mbalimbali pamoja na staili yake ya unenguaji, wakati kundi lake la TOT, lilipotumbuiza ukumbini hapo.
Baadhi ya wanamuziki wa TOT Taarab wakiimba kwa hamasa wakati kundi hilo la muziki wa taarab ilipotumbuiza kwenye ukumbi wa City Pub jijini Mbeya.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akimpongeza Bi. Khadija Kopa kwa umahiri wake wa kuimba taarab kwenye ukumbi wa City Pub Mbeya.
Umati wa mashabiki ukiwa umefurika kwenye ukumbi huo, wakati Malkia huyo wa Taarab, Bi. Khadija Kopa na kundi lake la TOT, likitoa burudani kwa wakazi wa Mbeya jiji la Mbeya.

No comments:

Post a Comment