TANGAZO


Thursday, February 20, 2014

Semina ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo

Mbunge Augostino Mrema, akizungumza na Wabunge Vita Kawawa wa Namtumbo (aliyemshika mkono), Abdulkarim Shah (kushoto) wa Mafia na  Januari Makamba wa Bumbuli, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mbunge Augostino Mrema, akizungumza na Wabunge Vita Kawawa wa Namtumbo (aliyemshika mkono), Abdulkarim Shah (kushoto) wa Mafia na  Januari Makamba wa Bumbuli, nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto), akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na Mbunge Samwel Sitta ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto), akijadiliana jambo na Zitto Kabwe, kabla ya kuanza kwa semina ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba. Wengine ni Dk. Hussein Ali Mwinyi, Profesa Mark Mwandosy, Margreth Sitta (juu kushoto) na Mussa Hajji Kombo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto), akizungumza jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndani ya ukumbi wa Bunge, wakati wa semina hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba, kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi huo wa Bunge leo. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba, kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi huo wa Bunge leo. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akitaka ufafanuzi kwa baadhi ya vifungu vya sheria hiyo, wakati wa semina hiyo leo. 

No comments:

Post a Comment