TANGAZO


Thursday, February 20, 2014

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha ashiriki maadhimisho ya mwaka mpya wa China

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Lizzy Lloyd akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa  Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Liu Youqing akitoa neno la shukrani kwa Benki ya Standard Chartered kwa kuandaa hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza kwenye halfa ya kuadhimisha mwaka mpya wa China, iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Dar es Salaam. Wakati wa hafla hiyo Balozi Gamaha aliupongeza Ubalozi wa China katika kusaidia na kuchangia maendeleo ya Tanzania. Pia Balozi Gamaha aliipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na Ubalozi wa China nchini katika kurahisisha  biashara kati ya Tanzania na China. 
Wageni waalikwa walioshiriki hafla hiyo.
Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari.
Balozi Gamaha (kulia) akimsikiliza Bw. Nathaniel Kaaya,  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla hiyo. Wengine wanaosikiliza  kutoka kushoto ni Bw. Iman Njalikai na Bw. Emmanuel Luangisa, Maafisa Mambo ya Nje. (Picha zote na Reginald Kisaka)

No comments:

Post a Comment