TANGAZO


Sunday, February 16, 2014

Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi azindua mpango endelevu kwa wakulima nchini

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akizindua  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania,anaeshuhudia kulia ni Diwani wa Kwadelo wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Bw. Omary Kariati aliyefanikisha mradi huo na kununua trekta (15) kwaajili ya wakulima nchini. Hafla hiyo imefanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiwasha Trekta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania, Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia kulia ni Diwani wa Kwadelo Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Bw. Omary Kariati aliyefanikisha mradi huo na kununua trekta (15) kwa ajili ya wakulima  nchini.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akiangalia moja ya Trekta kati ya(15) kabla  ya kuzindua mradi endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kwa ushirikiano na benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya Kwadelo Bw.Omary Kariati. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mpango maalumu  na  endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania na Diwani wa kata ya kwadelo wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Bw. Omary Kariati wapili kushoto. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wakuliama wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma wakimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi, (hayupo pichani) akiongea wakati wa makabidhiano rasmi wa Trekta (15), wakati akiuzindua mradi endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kwa ushirikiano na benki ya KCB Tanzania na Diwani wa Kata ya Kwadelo Bw. Omary Kariati.

Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa kibenki wa benki ya KCB Tanzania, Bw. Frank Nyabundege (kushoto), wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mpango maalumu  na endelevu wa kumuwezesha mkulima yeyote hapa nchi  kupata trekta  kwa bei nafuu kupitia ushirikiano wa benki ya KCB Tanzania na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Bw. Omary Kariati (kulia). Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment