TANGAZO


Sunday, February 23, 2014

Mugabe apeperusha mabofu 90

Rais Mugabe ametimiza miaka 90

Maelfu ya watu wa Zimbabwe wamehudhuria sherehe rasmi za siku ya kuzaliwa Rais Robert Mugabe.
Bwana Mugabe ambaye ameongoza nchi tangu mwaka wa 1980, alipeperusha mabofu 90 katika uwanja wa michezo wa Marondera, mashariki ya Harare.
Rais Mugabe, ambaye amerudi punde kutoka Singapore kwa matibabu, aliuambia umati kuwa ushindi aliopata kwenye uchaguzi wa mwaka jana ulishangaza nchi za magharibi zinazomlaumu.
Sherehe hiyo inakisiwa kugharimu dola milioni-moja na hivyo kuzusha malalamiko katika nchi ambayo ina matatizo ya kiuchumi.

No comments:

Post a Comment