TANGAZO


Thursday, February 20, 2014

Mashindano ya mpira wa Baseball kuanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam

 
 Katibu Mkuu Chama cha Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi (kushoto) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mashindano ya Kitaifa ya mchezo wa baseball yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari na Kutoka kulia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga.
 Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mashindano ya mchezo wa Baseball yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 na 23 mwezi huu katika shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi na anayemfuatia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga.
 Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (katikati) akitoa maelekezo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna mchezo wa Baseball unavyochezwa. Kushoto ni Mkufunzi wa mchezo huo Bi. Hellen Prosper Stima na kutoka kulia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga akifuatiwa na Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi
 Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (katikati) akitoa maelekezo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna mchezo wa Baseball unavyochezwa. Kushoto ni Mkufunzi wa mchezo huo Bi. Hellen Prosper Stima na kutoka kulia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga akifuatiwa na Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi.
Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (katikati) akimvalisha Mkufunzi Bi. Hellen Prosper Stima (kushoto) kifaa maalum cha kujikinga wakati wa kucheza mchezo wa baseball. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi.
Ofisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) (kushoto) Richard Mganga akiwaeleza waandishi wa habari juu ya mashindano ya mchezo wa baseball yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 na 23 katika shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari.
(Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)


Na Benedict Liwenga-MAELEZO

Mashindano ya mpira wa Baseball kuanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam

MASHINDANO ya Kimataifa ya kwanza na yakihistoria kufanyika hapa nchini ya  Mchezo wa Baseball yanatarajiwa kufanyika  tarehe 22 na 23 katika viwanja vya michezo vya shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wa chama cha Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi amesema kuwa mashindano hayo yatazishirikisha timu za sekondari za Sanya juu kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Londoni kutoka mkoa wa Ruvuma, Kibasila na Azania zote za jijini Dar es Salaam.
Mchimbi alisema nia ya mashindano hayo ni ni kumtafuta mshindi wa taifa katika ngazi ya shule za Sekondari ambapo washindi wa kwanza na wapili watapewa vikombe na washiriki wengine watapewa vyeti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mpira wa Baseball Africa (AFAB) Bw. Shinya Tomonari amesema kwamba amekuwa akifundisha nchi mbali mbali Afrika ikiwemo nchi ya Ghana na amefungua Chama kinachoshughulikia mpira wa magongo ambacho kwa sasa kimeenea nchi nyingi zikiwemo Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Nigeria, Burkina Faso, Lesotho na Zambia, hivyo amevutiwa kuja Tanzania na kuanzisha mpira wa magongo hasa kwa vijana wa shule hapa nchini.
“Matamanio yangu ni kuanzisha mpira wa magongo kwa watanzania na sana sana kwa vijana wa shule, hivyo basi nimeshauriwa kuanza na shule za Sekondari za Kibasila na Azania”. Alisema Bwana Tomonari.
Ameongeza kuwa Chama hicho kinatoa mchango mkubwa wa vifaa vya michezo kupitia shirika la Kijapan (JICA) na kupitia JICA baadhi ya walimu na wakufunzi walianzisha timu za mpira wa magongo ambapo mpaka sasa kuna timu mbili zilizoanzishwa moja iliyoko Sanya Juu mkoani Kilimanjaro na nyingine ipo Songea mkoani Ruvuma. Pia kuna timu nyingine ambayo iko jijini Mwanza katika Shule ya St. Marys.

No comments:

Post a Comment